Wazayuni wahamakishwa na mapatano baina ya Iran na Saudia
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i95002-wazayuni_wahamakishwa_na_mapatano_baina_ya_iran_na_saudia
Makubaliano yaliyofikiwa siku ya Ijumaa ya mjini Beijing China kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Saudi Arabia yalipokelewa kwa shangwe na nchi za eneo na kwingineko, lakini yamewahamakisha Wazayuni.
(last modified 2026-05-20T03:07:53+00:00 )
Mar 12, 2023 04:43 UTC
  • Wazayuni wahamakishwa na mapatano baina ya Iran na Saudia

Makubaliano yaliyofikiwa siku ya Ijumaa ya mjini Beijing China kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Saudi Arabia yalipokelewa kwa shangwe na nchi za eneo na kwingineko, lakini yamewahamakisha Wazayuni.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Fars, Ijumaa ya tarehe 19 Machi kulitangazwa habari kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Saudi Arabia zimeafikiana kurejesha uhusiano wa kidiplomasia ndani ya miezi miwili ijayo.

Uhusiano huo ambao Saudia ndio iliyoukata kwa upande mmoja mwezi Januari 2015 kufuatia maandamano yaliyotokea mbele ya ubalozi wa nchi hiyo mjini Tehran na Ubalozi wake mdogo mjini Mashhad hapa Iran yaliyotokana na hatua ya Riyadh ya kumnyonga Sheikh Nimr, utaanza tena baada ya kusimama kwa miaka saba.

Bendera ya utawala wa Kizayuni wa Israel

 

Nchi, duru, taasisi na mirengo mbalimbali ya kieneo na kimataifa imeonesha hisia zao nzuri kuhusu makubaliano hayo ya kuanzishwa tena uhusiano wa kidiplomasia baina ya Iran na Saudi Arabia kiasi kwamba hata mmoja wa watu maarufu wa Marekani amedai kuwa Washington inakaribisha juhudi za kutatuliwa mgogoro wa Yemen, lakini kwa utawala wa Kizayuni, hatua hiyo ni pigo kubwa zaidi kwake na umeshindwa kuficha hamaki zake.

Naftali Bennett, Waziri Mkuu wa zamani wa utawala wa Kizayuni amesema: "Kuhuishwa uhusiano kati ya Iran na Saudi Arabia ni hatari kubwa kwa Israel na ni ushindi wa kisiasa kwa Iran. Hili ni pigo baya kwa juhudi za kuunda muungano wa kikanda ulio dhidi ya Iran."

Naye Yair Lapid, waziri wa zamani wa mambo ya nje wa utawala wa Kizayuni ameandika kwenye mtandao wa kijamii Twitter: "Makubaliano kati ya Iran na Saudi Arabia ni sawa na kushindwa kabisa na ni hatari kwa sera za kigeni za Israel. Hii ina maana ya kuanguka muungano wa kikanda ambao ulianzishwa dhidi ya Iran."