-
Iran yalaani kitendo cha Canada kuzuia Wairani nchini humo kupiga kura uchaguzi wa rais
Jun 11, 2021 08:05Msemaji wa Tume ya Uchaguzi ya Iran amesema hatua ya Canada ya kukataa kutoa ushirikiano ili kuhakikisha Wairani wanaoishi Canada wanapiga kura katika uchaguzi wa rais wa Iran, ni ukiukwaji wa sheria za kimataifa.
-
Uchaguzi wa Rais wa Iran kufanyika London, miji mingine 6 ya Uingereza
Jun 11, 2021 03:29Ubalozi wa Iran nchini Uingereza umesema wananchi wa Iran walioko katika nchi hiyo ya bara Ulaya watakuwa na fursa ya kupiga kura katika uchaguzi wa 13 wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu katika mji mkuu London, na miji mingine sita mikubwa ya nchi hiyo.
-
Pentagon yaingiwa na kiwewe baada ya manowari za Iran kuwasili Atlantic
Jun 10, 2021 22:22Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) imeingiwa na kiwewe na wahaka mkubwa baada ya msafara wa meli za kijeshi za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwasili katika Bahari ya Atlantic pasi na kupitia katika bandari za nchi nyingine kwa mara ya kwanza katika historia.
-
Iran yaitaka IAEA kuacha sera za upendeleo
Jun 10, 2021 21:44Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Iran katika jumuiya za kimataifa huko Vienna nchini Austria ameutaka Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) kuacha sera za upendeleo.
-
Rouhani: Iran inaunda vituo 2 vya nishati ya nyuklia kwa ushirikiano na Russia
Jun 10, 2021 08:21Rais Hassan Rouhani wa Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu imeanza ujenzi wa vinu viwili vipya vya nishati ya nyuklia kwa ushirikiano na Russia.
-
Araqchi: Masuala muhimu katika mazungumzo ya nyuklia yangali yamesalia
Jun 09, 2021 22:13Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Anayehusika na Masuala ya Kisiasa amesema kuwa, masuala muhimu yangali yamesalia katika mazungumzo ya nyuklia kati ya Iran na kundi la 4+1 na maamuzi yanapaswa kuchukuliwa katika uwanja huo.
-
Mwakilishi wa Hamas nchini Iran: Utawala wa Kizayuni hauaminiki kwa ahadi yoyote
Jun 09, 2021 21:58Mwakilishi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) nchini Iran amesisitiza kuwa, utawala wa Kizayuni si wa kuaminiwa kwa ahadi yoyote lakini katika vita vya siku 12 utawala huo umelazimika kukubali masharti ya wanamapambano wa Palestina.
-
Mgombea urais Iran aahidi kutumia vizuri fursa za kiuchumi za Afrika iwapo atachaguliwa
Jun 09, 2021 08:11Mgombea mmoja katika uchaguzi wa 13 wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, iwapo atachaguliwa, serikali yake itatumia vizuri sana uwezo wa kila namna wa kiuchumi wa nchi za Afrika katika ustawi wa pande mbili na pande kadhaa.
-
Rais Rouhani: Uwezo wa Iran wa kuzalisha bidhaa za petrokemikali umeongezeka maradufu
Jun 09, 2021 07:45Rais Hassan Rouhani amesema kuwa uwezo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wa kuzalisha bidhaa za petrokemikali umeongezeka maradufu hivi sasa.
-
Zarif: Kuna wajibu wa kuodolewa vikwazo vyote dhidi ya Yemen, haraka iwezekanavyo
Jun 08, 2021 21:58Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amekutana na mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Yemen na kusema kuwa, kuna wajibu na udharura wa kuondolewa haraka vikwazo walivyowekewa wananchi wa Yemen.