-
Iran: Taifa la Palestina halina chaguo jingine ghairi ya muqawama
Jun 10, 2020 22:58Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran katika masuala ya Sheria na Kimataifa amesema wananchi wa Palestina hawana chaguo jingine isipokuwa mapambano na muqawama ili waweze kupata haki zao za msingi na kujiamulia mustakabali wao.
-
"Kujiepushe na mifarakano na kushambuliana, hatua ya kwanza ya kujenga Umoja wa Kiislamu"
Jun 10, 2020 21:54Katibu Mkuu wa Baraza la Kimataifa la Kukurubisha Pamoja Madhehebu Mbalimbali ya Kiislamu amesema kuwa, jengo la umoja na mshikamano baina ya Waislamu linahitajia kuchukuliwa hatua kadhaa za utangulizi ambapo hatua ya kwanza kabisa muhimu ni kujiweka mbali na mifarakano na kuacha kushambuliana mataifa ya Waislamu.
-
Rouhani: Marekani inapanga njama kuzuia kuondolewa vikwazo vya silaha dhidi ya Iran
Jun 10, 2020 08:24Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria kufutwa vikwazo vyote vya silaha dhidi ya Iran baadaye mwezi Oktoba mwaka huu na kusema Marekani imeghadhabishwa na mpango wa kufutwa vikwazo hivyo na sasa inapanga njama ya kutaka vikwazo hivyo visalie.
-
Meja Jenerali Salami: Nembo za dola kubwa la Marekani zameanza kuporomoka
Jun 10, 2020 08:19Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema mienendo ya nchi za dunia inabadilika na kuongeza kuwa: "Nembo zote ambazo Marekani imekuwa ikizitumia kujiarifisha kama dola kubwa duniani na kuzitumia kuwasilisha taswira isiyo ya kweli sasa zimeanza kusambaratika."
-
Mousavi: Iran haitasalimu amri mbele ya vikwazo vya kukaririwa vya Marekani
Jun 10, 2020 03:50Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa viongozi wa Marekani wanajisumbua bure kwa vikwazo hivyo vipya na kwamba Iran katu haitasalimu amri mbele ya vikwazo na mashinikizo ya aina hii. Sayyid Abbas Mousavi ameyasema hayo kufuatia hatua ya Marekani ya kuyawekea vikwazo vipya makampuni ya meli na meli za kubeba mafuta za Iran.
-
Jasusi wa CIA na Mossad ahukumiwa kifo nchini Iran
Jun 09, 2020 06:48Msemaji wa Idara ya Mahakama ya Iran amesema kuwa, jasusi wa Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) na shirika la ujasusi la Israel, Mossad hapa nchini, amehukumiwa kifo.
-
"Hatukuiruhusu Marekani ikandamize kwa goti uzalishaji nchini Iran"
Jun 09, 2020 03:42Rais Hassan Rouhani wa Iran amesema kaulimbiu ya 'Ustawi mkubwa katika Uzalishaji' ndiyo suluhu ya matatizo yote ya kiuchumi ya Jamhuri ya Kiislamu, na hilo litaafikiwa kwa ushirikiano na jitihada za pamoja.
-
Kiongozi Muadhamu awashukuru wafanyakazi wa meli za mafuta za Iran zilizotumwa Venezuela
Jun 08, 2020 23:10Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametuma ujumbe kufuatia harakati ya Kijihadi ya makamanda na wafanyakazi wa meli za mafuta za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambazo zilibeba shehena za bidhaa za petroli na kuzifikisha nchini Venezuela.
-
Mafanikio ya tiba ya Iran katika kukabiliana na corona; fakhari ya kubakia milele
Jun 08, 2020 05:52Jamhuri ya Kiislamu ya Iran umefanikiwa vizuri sana katika vita dhidi ya ugonjwa wa COVID-19 licha ya kuweko matatizo na mashinikizo ya kigeni. Iran imepata mafanikio ya kujivunia na fakhari za kubakia milele katika juhudi zake hizo.
-
Rouhani: Ramadhan Shalah alisabilia maisha yake kupambana na Wazayuni
Jun 07, 2020 22:26Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria tukio la kuaga dunia katibu mkuu wa zamani wa Harakati ya Jihad Islami ya Palestina na kusema kuwa, shakhsia huyo alisabilia maisha yake yote katika kupambana na utawala wa Kizayuni wa Israel.