Rouhani: Ramadhan Shalah alisabilia maisha yake kupambana na Wazayuni
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i61480-rouhani_ramadhan_shalah_alisabilia_maisha_yake_kupambana_na_wazayuni
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria tukio la kuaga dunia katibu mkuu wa zamani wa Harakati ya Jihad Islami ya Palestina na kusema kuwa, shakhsia huyo alisabilia maisha yake yote katika kupambana na utawala wa Kizayuni wa Israel.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Jun 07, 2020 22:26 UTC
  • Rouhani: Ramadhan Shalah alisabilia maisha yake kupambana na Wazayuni

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria tukio la kuaga dunia katibu mkuu wa zamani wa Harakati ya Jihad Islami ya Palestina na kusema kuwa, shakhsia huyo alisabilia maisha yake yote katika kupambana na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Katika salamu zake za rambirambi jana Jumapili, Rais Rouhani amesema, "mwanafikra na mchapakazi huyu mwanajihadi alijitolea maisha yake yote yaliyojaa baraka katika mapambano dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel, sanjari na kulinda thamani za wananchi madhulumu wa Palestina."

Dakta Rouhani amemtaja mwanaharakati huyo kama shakhsia aliyeacha msingi madhubuti kwa vizazi vijavyo katika uga wa jihadi na muqawama.

Rais wa Iran amesema kazi na jitihada za Ramadhan Abdullah Shalah, Katibu mkuu wa zamani wa Harakati ya Jihad Islami ya Palestina kwa ajili ya Wapalestina zitasalia katika madaftari ya historia na kumbukumbu.

Marehemu Ramadhan Abdullah Shalah

Mapema jana pia, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alituma salamu za rambi rambi kufuatia kuaga dunia Shalah na kusema kuwa, Katibu Mkuu huyo wa zamani wa Jihad Islami ya Palestina alikuwa mtu mwenye khushuu, msomi, mwanafikra aliyekuwa na fikra za kukurubisha madhehebu za Kiislamu na aliyefahamu kwa kina matukio ya kieneo na dunia.

Ramadhan Shalah aliaga dunia juzi Jumamosi akiwa hospitalini katika mji wa Gaza, baada ya kusumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu.