Iran: Taifa la Palestina halina chaguo jingine ghairi ya muqawama
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i61531-iran_taifa_la_palestina_halina_chaguo_jingine_ghairi_ya_muqawama
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran katika masuala ya Sheria na Kimataifa amesema wananchi wa Palestina hawana chaguo jingine isipokuwa mapambano na muqawama ili waweze kupata haki zao za msingi na kujiamulia mustakabali wao.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 10, 2020 22:58 UTC
  • Iran: Taifa la Palestina halina chaguo jingine ghairi ya muqawama

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran katika masuala ya Sheria na Kimataifa amesema wananchi wa Palestina hawana chaguo jingine isipokuwa mapambano na muqawama ili waweze kupata haki zao za msingi na kujiamulia mustakabali wao.

Mohsen Baharvand alisema hayo jana Jumatano katika mkutano uliofanyika kwa njia ya inteneti uliotishwa na Kamati Kuu ya Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) ngazi ya mawaziri wa mambo ya nje.

Mkutano huo umeitishwa kwa lengo la kujadili hatua za utawala wa Kizayuni wa Israel kunyakua ardhi zaidi za Wapalestina katika mji wa Quds (Jerusalem) na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Baharvand ambaye ameiwakilisha Iran katika mkutano huo kufuatia ombi la Mamlaka ya Ndani ya Palestina na Mkurugenzi Mkuu, Yousef Al-Othaimeen ameeleza bayana kuwa: Jamhuri ya Kiislamu itaendelea kuunga mkono kadhia ya Palestina kwa hali zote. Ulimwengu wa Kiislamu unapaswa kutafakari juu ya stratajia mpya itakayowadhaminia Wapalestina haki yao ya msingi ya kujiamulia wenyewe mustakabali wa taifa lao.

Harakati za muqawama Asia Magharibi

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran katika masuala ya Sheria na Kimataifa amesisitiza kuwa, mataifa ya Kiislamu yanapaswa kuafikiana juu ya sera itakayozaa matunda, hususan wakati huu ambapo Marekani na utawala wa Kizayuni zimedhihirisha wazi unafiki wao na nia yao mbaya ya kukwamisha uundwaji wa taifa huru la Palestina.

Kadhalika amelaani vikali hatua ya utawala huo pandikizi ya kuuhamishia mji mkuu wake Baitul Muqaddas kutoka Tel Aviv, na vile vile mpango wake wa kutaka kuyaunganisha baadhi ya maeneo ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel).