-
Wazayuni wafanya mashambulizi makubwa katika hospitali moja huko mjini Beirut
Oct 05, 2024 09:08Wavamizi wa Kizayuni wamelenga hospitali ya Bint Jbeil iliyoko kusini mwa Lebanon.
-
Asilimia 6 ya wakazi wa Gaza wameuawa au kujeruhiwa katika mwaka mmoja wa mauaji ya kimbari ya Israel
Oct 05, 2024 08:52Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa kufuatia mwaka mmoja wa mauaji ya kimbari yanayoendelezwa na utawala wa Kizayuni wa Israel, asilimia 6 ya wakazi wa Gaza wameuawa au kujeruhiwa.
-
Hizbullah yavurumisha makombora kwenye maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na Israel
Oct 05, 2024 02:31Duru za habari zimeripoti kuwa, makombora na maroketi 70 yamerushwa kutoka Lebanon kuelekea kaskazini mwa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu (Israel).
-
Shambulio la ndege za kivita za utawala wa Kizayuni katika viunga vya kusini mwa Beirut
Oct 05, 2024 02:13Vyanzo vya habari vmeripoti leo Jumamosi asubuhi kwamba, ndege za kivita za utawala wa Kizayuni zimeshambulia vikali kitongoji cha "al-Abyadh" katika viunga vya kusini mwa mji wa Beirut.
-
Oman: Badala ya kulaani hatua ya Iran, komesheni Israel kuikalia kwa mabavu ardhi ya Palestina
Oct 05, 2024 00:14Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman amesema, badala ya kulaani hatua ya Iran, ukomeshwe ukaliaji ardhi ya Palestiina kwa mabavu unaofanywa na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.
-
Duru iliyo karibu na Hizbullah: Mwili wa Shahidi Sayyid Nasrullah umezikwa kwa muda 'sehemu isiyojulikana'
Oct 04, 2024 06:54Duru iliyo karibu na Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imetangaza kuwa mwili wa Shahidi Sayyid Hassan Nasrullah umezikwa kwa muda katika sehemu isiyojulikana.
-
Mauaji ya Sayyid Hassan Nasrullah yamekuwa na taathira hasi ya kinyume cha matarajio kwa adui
Oct 04, 2024 06:14Mwakilishi wa Harakati ya Hizbullah katika Bunge la Lebanon amesema, kuuawa shahidi Sayyid Hassan Nasrullah kumeutia moyo na kuupa ari kubwa Mhimili wa Muqawama na kuwa na taathira hasi na kinyume na iliyotarajiwa kwa utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Zawadi ya tunu ya HAMAS kwa Sayyid Hassan Nasrullah + VIDEO
Oct 04, 2024 04:29Brigedi za Izzuddin Qassam, Tawi la Kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS zimesambaza mkanda wa video na ndani yake wanatangaza kuwa operesheni hiyo ni zawadi kwa shahid wa Muqawama, Sayyid Hassan Nasrullah. Mkanda huo unaonesha mtego kabambe waliowawekea wanajeshi katili wa Israel na vifaru na mabuldoza yao na namna vinavyoteketezwa kimoja baada ya kingine huko Khan Yunus, katika Ukanda wa Ghaza.
-
Israel yaendelea kumwaga damu za Walebanon mjini Beirut
Oct 04, 2024 03:43Wizara ya Afya ya Lebanon imesema takriban watu 37 wameuawa shahidi huku wengine zaidi ya 150 wakijeruhiwa katika mashambulizi mapya ya anga ya utawala haramu wa Israel, huku uchokozi usio na kikomo wa utawala huo katili dhidi ya Lebanon ukiendelea.
-
Ansarullah: Nasrullah alizima njama za Wazayuni katika eneo
Oct 03, 2024 23:44Kiongozi wa Harakati ya Muqawama ya Ansarullah ya Yemen sanjari na kutoa pongezi na mkono wa pole kufuatia kuuawa shahidi Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon, amesema Sayyid Hassan Nasrullah alitibua njama za Israel na kuusababishia utawala huo dhalimu vipigo vya fedheha.