Shambulio la ndege za kivita za utawala wa Kizayuni katika viunga vya kusini mwa Beirut
Vyanzo vya habari vmeripoti leo Jumamosi asubuhi kwamba, ndege za kivita za utawala wa Kizayuni zimeshambulia vikali kitongoji cha "al-Abyadh" katika viunga vya kusini mwa mji wa Beirut.
Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA, jeshi la utawala huo bado halijatangaza lengo la kufanya mashambulizi hayo makali ya mabomu katika eneo hilo.
Vile vile, ndege zisizo na rubani za utawala wa Kizayuni zimelenga jengo moja katika kambi ya wakimbizi ya al-Badawi katika mji wa Tripoli.
Katika shambulio hilo nyumba moja ya makazi imeshambuliwa na ndege isiyo na rubani na kuharibiwa kabisa.
Kituo cha habari cha Al Jazeera vile vile kimeripoti kuuawa shahidi watu wanne 4 na kujeruhiwa wengine kadhaa katika shambulio hilo.
Baadhi ya vyombo vya habari vimesema kuwa shambulio hilo limefanyika kwa shabaha ya kumuua kigaidi shakhsia mmoja wa Palestina au Lebanon katika kambi ya al-Badawi katika mji wa Tripoli ulioko kaskazini mwa Lebanon.
Tarehe 23 Septemba, jeshi katili la utawala wa Israel lilianzisha mashambulizi makali katika maeneo mbalimbali ya kusini mwa Lebanon, mashambuli ambayo yangali yanaendelea hadi sasa.