-
Mazungumzo ya Doha: Iran yasema Israel, Marekani zinahadaa na haziaminiki
Aug 17, 2024 01:09Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ametoa kauli kuhusu mazungumzo ya kusitisha mapigano Gaza yanayoendelea jijini Doha nchini Qatar, ambapo ameonya kuhusu "udanganyifu na ukosefu wa uaminifu" wa utawala dhalimu wa Israel na muungaji mkono wake muhimu zaidi, Marekani.
-
Mizozo katika safu za Wazayuni, Ben-Gvir aanzisha jeshi lake maalumu Ukingo wa Magharibi
Aug 17, 2024 00:54Viongozi wa utawala wa Kizayuni ni viumbe woga mno wanaopenda maisha kupindukia kiasi kwamba, kwa kuogopa vipigo vya muqawama na mizozo ya kisiasa na kijamii ndani ya Israel, baadhi yao kama Itamar Ben-Gvir wameunda vikosi maalumu vya kijeshi kuwalinda na kuwashinda nguvu mahasimu wao ndani ya utawala wa Kizayuni.
-
Hizbullah: Hakuna shaka tutatoa jibu kwa mauaji ya kigaidi ya Israel
Aug 16, 2024 07:13Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebanon kwa mara nyingine tena imesisitiza azma yake ya kulipiza kisasi cha mauaji ya Israel dhidi ya kamanda mwandamizi wa kundi hilo la Mapambano ya Kiislamu, licha ya juhudi za Marekani za kuukingia kifua utawala huo wa Kizayuni na kutaka kuuepusha na matokeo mabaya ya jinai zake.
-
Hamas: Usitishaji mapigano lazima uhusishe kuondoka kikamilifu Israel Ukanda wa Gaza
Aug 16, 2024 04:25Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) kwa mara nyingine tena imesisitiza kuwa makubaliano yoyote na Israel lazima yahakikishe usitishaji kamili wa vita huko Gaza, kuondoka kikamili majeshi ya Israel katika eneo hilo na makubaliano ya kubadilishana wafungwa.
-
Israel yapata hasara ya dola bilioni 67 kutokana na vita vya Gaza
Aug 16, 2024 04:06Wachumi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamefichua hasara kubwa za kiuchumi za vita vya Gaza kwa utawala huo na kusema, uchumi wa Israel unakabiliwa na mgogoro usioweza kudhibitiwa.
-
Umoja wa Mataifa kwa mara nyingine wataka kukomeshwa vita Gaza
Aug 16, 2024 00:53Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, kuongezeka watu wanaouawa huko Gaza kunatisha na hivyo ametoa mwito wa kukomeshwa mara moja ukatili huo.
-
Israel inashinikiza ICC ifute waranti wa kukamatwa Netanyahu
Aug 15, 2024 04:13Utawala wa Kizayuni umeripotiwa kushadidisha 'mashinikizo ya kidiplomasia' dhidi ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC ambayo inataka kutolewa waranti wa kukamatwa Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu na waziri wa vita wa utawala huo haramu, Yoav Gallant, kwa sababu ya kuhusika na uhalifu wa kivita.
-
Hali ya kutisha ya zama za mwisho huko Gaza
Aug 15, 2024 01:05Huku nchi za Magharibi zikiunga mkono jinai zinazoongezeka kila siku za utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina hasa katika kuwalazimisha watu wa Gaza kuyahama makazi yao, weledi wa mambo wanasema wigo wa jinai hizo unaweza kuzikumba nchi hizo pia baada ya muda usio mrefu.
-
Bin Salman ahofia kuuawa kwa kufuatilia mpango wa kuanzishwa uhusiano rasmi kati ya Saudia na Israel
Aug 15, 2024 00:15Mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman ameripotiwa kuwa anahofia "kuuawa" kwa sababu ya juhudi zake za kutaka kuhakikisha ufalme huo unaanzisha uhusiano rasmi na utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Muqawama Iraq: Jibu la Iran dhidi ya Israel litakuwa la nguvu
Aug 14, 2024 23:16Mkuu wa Baraza la Kisiasa la Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya al-Nujabaa ya Iraq amesema jibu tarajiwa la Iran kwa mauaji ya kigaidi yaliyofanywa mwezi uliopita na utawala wa Kizayuni dhidi ya Ismail Haniyah, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS litakuwa la nguvu, lenye taathira na la kimahesabu.