-
Erdogan: Iwe ni karibuni au baadaye, Israel italipa kwa mauaji ya kimbari inayoendeleza Ghaza
Oct 08, 2024 22:59Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki amesema, iwe iwavyo utawala wa Kizayuni wa Israel utalipa kwa mauaji ya kimbari ambayo umekuwa ukiendelea kuyafanya katika Ukanda wa Ghaza kwa mwaka mmoja sasa.
-
Ripoti: US imetumia $ bilioni 22 kuisaidia kijeshi Israel tangu Oktoba 7, kiwango halisi ni zaidi
Oct 08, 2024 22:57Marekani imetumia zaidi ya dola bilioni 22 kwa ajili ya misaada ya kijeshi inayoupatia utawala wa Kizayuni wa Israel na kufadhili uvamizi na mashambulio yaliyofanywa na utawala huo haramu katika eneo hili kwa kipindi cha mwaka mmoja sasa.
-
Korea Kusini yadai: Askari wa Korea Kaskazini wanapigana bega kwa bega na Russia Ukraine
Oct 08, 2024 22:55Waziri wa Ulinzi wa Korea Kusini amesema, inavyoonekana wanajeshi wa Korea Kaskazini wanapigana bega kwa bega na wanajeshi wa Russia nchini Ukraine.
-
Mkurugenzi Mkuu wa IAEA akosoa vikali shambulio dhidi ya wafanyakazi wa vituo vya nyuklia
Oct 08, 2024 02:25Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) amelaani vikali shambulio na vitisho dhidi ya wafanyakazi wa vituo vya nyuklia na kusema kuwa, ni ukiukaji wa wazi wa kanuni za kimsingi za usalama wa nyuklia.
-
UN: Maisha ya maelfu ya wanawake Gaza yako hatarini huku Israel ikiendeleza vita
Oct 07, 2024 23:32Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na kazi ya usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake linasema maelfu ya wanawake wanakabiliwa na hatari za kiafya zinazohatarisha maisha katika Ukanda wa Gaza, ambapo zaidi ya Wapalestina 42,000 wameuawa kutokana na vita vya mauaji ya kimbari vinavyowendelezwa na utawala katili wa Israel.
-
SEPAH: Tumejiandaa kikamilifu kukabiliana na jinai yoyote ya adui
Oct 07, 2024 07:32Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH amesema kuwa jeshi hilo linajivunia nishani ya Fat'h ambayo Amirijeshi Mkuu wa majeshi yote ya Iran amemtunuku Amir Ali Hajizadeh, Kamanda wa Kikosi cha Anga na Anga za Mbali cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kwamba jeshi hilo imara la Iran limejiandaa kikamilifu kupambana na jinai yoyote ile ya adui.
-
Sera zinazokinzana za Macron kuhusiana na mashambulizi wa Wazayuni nchini Lebanon
Oct 07, 2024 07:22Wito wa Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, wa kusitishwa msaada wa silaha kwa utawala bandia na ghasibu wa Israel umefuatiwa na jibu kali la Waziri Mkuu wa utawala huo, Benjamin Netanyahu.
-
Vyombo vya habari vya michezo duniani vyalalamikia kimya cha FIFA mbele ya jinai za Israel
Oct 06, 2024 08:04Aghalabu ya vyombo vya habari mashuhuri vya michezo duniani vimekosoa kimya, mchezo wa kisiasa na unafiki wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) mkabala wa jinai na mauaji ya kimbari yanayofanywa na Israel.
-
Katibu Mkuu wa UN: Sasa ni wakati wa kunyamazishwa sauti za bunduki Mashariki ya Kati
Oct 06, 2024 03:59Katika mkesha wa kumbukumbu ya mwaka wa kwanza wa mashambulizi ya Oktoba 7, 2023, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa wito wa kukomesha mara moja "umwagaji damu na ukatili wa kutisha" katika ukanda wa Gaza na Lebanon, kunyamazisha sauti za bunduki na kurejeshwa amani katika eneo hilo.
-
Wamagharibi nao wamechoshwa na jinai za Israel, Macron ataka iwekewe vikwazo vya silaha
Oct 06, 2024 03:56Rais wa Ufaransa, Emanuel Macron, ametoa wito wa "kuwekewa vikwazo vya silaha" utawala wa Israel kutokana na vita na mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala huo dhidi ya Ukanda wa Gaza.