-
Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu latahadharisha kuhusu hali mbaya ya mji wa Rafah
May 26, 2024 03:33Mkuu wa Shirikisho la Kimataifa la taasisi za Msalaba Mwekundu na Mwezi Mwekundu (IFRC) ametahadharisha kuhusu hali ya kibinadamu katika mji wa Rafah na kusema kuwa hali ya mambo katika eneo la kusini mwa Ukanda wa Gaza ni mbaya sana.
-
WHO: Kwa miaka miwili, Covid-19 iliua karibu watu milioni 13 duniani
May 26, 2024 01:09Shirika la Afya Duniani (WHO) limeeleza katika ripoti kuwa, watu wapatao milioni 13 walifariki dunia wakati wa janga la Covid-19, huku kirusi cha ugonjwa huo kikigeuka haraka kuwa chanzo kikuu cha vifo katika bara la Amerika.
-
UN yaitaka Israel isimamishe mashambulio Rafah kama ilivyoagizwa na ICJ
May 25, 2024 07:36Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameutaka utawala haramu wa Israel uheshimu na utekeleza amri ya kusitisha operesheni za kijeshi mjini Rafah, kama ilivyoagizwa na mahakama kuu ya Umoja wa Mataifa.
-
Borrell: Umoja wa Ulaya uchague ama vita au Israel
May 25, 2024 07:33Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya amesema EU inapasa kuweka bayana msimamo wake kuhusu uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) wa kuutaka utawala wa Israel usitishe mara moja mashambulizi yake ya kijeshi mjini Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza.
-
Maporomoko ya udongo yaua mamia ya watu New Papua Guinea
May 25, 2024 07:32Mamia ya watu wameripotiwa kuaga dunia kutokana na mafuriko na maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha huko Papua New Guinea (PNG).
-
Ripota Maalumu wa UN ataka Israel iwekewe vikwazo
May 25, 2024 07:32Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu ametoa mwito wa kuwekewa vikwazo utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
UN: Warohingya 45,000 wakimbilia katika maeneo karibu na mpaka wa Bangladesh
May 24, 2024 22:35Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa jana Ijumaa ilieleza kuwa Waislamu wa Rohngya wasiopungua elfu 45 wamekimbilia katika maeneo karibu na mpaka wa Bangladesha baada ya kuripotiwa mapigano.
-
Vikwazo vya China dhidi ya Marekani
May 24, 2024 22:34ikiwa ni katika kukabiliana na mashinikizo ya vikwazo na pia uuzaji wa silaha za Marekani katika eneo la Taiwan, China imepitisha vikwazo dhidi ya makampuni 12 yanayuhusiana na viwanda vya kijeshi vya Marekani na wasimamizi wakuu wa mashirika hayo.
-
Seneta wa Marekani: Vikwazo vyetu dhidi ya Iran, Russia na China havina tija yoyote
May 24, 2024 06:49Seneta Rand Paul wa chama cha Republican nchini Marekani amesema sera ya Washington ya kuendelea kushadidisha vikwazo dhidi ya Russia, China na Iran haina tija yoyote.
-
ICJ yaiamuru Israel isimamishe mashambulio yake Rafah, Ghaza
May 24, 2024 12:50Mahakama ya Umoja wa Mataifa imeuamuru utawala wa Kizayuni wa Israel usitishe mara moja mashambulizi yake katika mji wa kusini mwa Ghaza wa Rafah na kujiondoa katika eneo hilo, kufuatia kesi iliyowasilishwa na Afrika Kusini ikiishutumu Israel kwa kufanya mauaji ya kimbari, na kuielezea hali hiyo kuwa ni hatari kubwa kwa wakazi wa Palestina.