May 26, 2024 07:03 UTC
  • Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu latahadharisha kuhusu hali mbaya ya mji wa Rafah

Mkuu wa Shirikisho la Kimataifa la taasisi za Msalaba Mwekundu na Mwezi Mwekundu (IFRC) ametahadharisha kuhusu hali ya kibinadamu katika mji wa Rafah na kusema kuwa hali ya mambo katika eneo la kusini mwa Ukanda wa Gaza ni mbaya sana.

Francesco Rocca ameeleza kuwa hali ya kibinadamu katika mji wa Rafah ni mbaya sana na kila siku hali ya mambo inazidi kuwa mbaya. Rocca pia amebainisha wasiwasi wake kutokana na hali ya mgogoro inayovunja matumaini na kushtadi hali mbaya ya kibinadamu huko Ukanda wa Gaza.  

Francesco Rocca 

Huko nyuma Ashraf al Qudra Msemaji wa Wizara ya Afya ya Palestina katika Ukanda wa Gaza alieleza kuwa zaidi ya wagonjwa 20,000 wanaougua saratani, magonjwa ya moyo na damu wanasubiri kufunguliwa kivuko cha Rafah huko Gaza wakikabiliwa na hali ngumu kutokana na kukaliwa kwa mabavu, kuzingirwa na mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na utawala wa Kizayuni katika ukanda huo. 

Msemaji wa Wizara ya Afya ya Palestina katika Ukanda wa Gaza ameongeza kuwa taasisi za kimataifa zinafanya kazi kwa mwendo wa kinyonga katika kushughulikia matatizo ya wakazi wa ukanda huo licha ya wakazi wa eneo hilo kukabiliwa na mauaji ya kimbari na kubomolewa nyumba na miundombinu katika ukanda huo.