-
Maelfu waandamana Kashmir kutoa heshima na kumuomboleza Shahidi Rais Raisi
May 24, 2024 07:25Maelfu ya watu wameandamana katika eneo la Kashmir kutoa heshima zao na kuomboleza kifo cha marehemu Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Shahidi Sayyid Ebrahim Raeisi, ambaye alikufa shahidi katika ajali ya helikopta pamoja na maafisa wengine kadhaa mapema wiki hii.
-
Mashirika zaidi ya 120 ya haki za binadamu yamtaka Biden aheshimu uhuru wa ICC
May 24, 2024 06:50Jumla ya mashirika 121 ya kutetea haki za binadamu pamoja na ya kiraia yamemtaka Rais Joe Biden wa Marekani aheshimu na kuunga mkono uhuru wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) na kukemea vitisho vya uwekaji vikwazo vinavyotolewa na viongozi wa Maarekani dhidi ya maafisa wa mahakama hiyo.
-
Upinzani wa Marekani dhidi ya hatua ya nchi za Ulaya ya kulitambua taifa la Palestina
May 24, 2024 04:25Siku ya Jumatano, Ikulu ya Marekani ailitoa taarifa ya kuunga mkono kwa pande zote utawala haramu Israel na kusema kuwa Rais Biden anaamini kwamba taifa la Palestina linapaswa kuanzishwa kupitia mazungumzo na si kutambuliwa kwa upande mmoja na baadhi ya nchi.
-
Guterres: Afrika ina mchango muhimu kwa amani na usalama wa dunia
May 24, 2024 03:52Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameashiria nafasi muhimu ya Afrika katika kuufanya ulimwengu uwe pahala pazuri na salama na kusisitiza kuwa, "Wakati umefika wa kuanika uwezo wa amani wa Afrika."
-
ICJ kutoa uamuzi wake kuhusu ombi la Afrika Kusini la kutaka Israel isitishe vita Gaza
May 23, 2024 23:07Mahakama ya Kimataifa ya Haki (OCJ) leo Ijumaa inatarajiwa uamuzi wake kuhusiana na ombi la Afrika Kusini la kutaka Israel kushinikizwa kutekeleza wito wa usitishwaji wa mapigano katika ukanda wa Gaza huko Palestina.
-
Baada ya Colombia kuvunja uhusiano na Israel, sasa kufungua ubalozi wake Ramallah
May 23, 2024 23:06Baada ya Colombia hivi karibuni kuvunja uhusiano wake na utawala haramu wa Israel, nchi hiyo sasa imetangaza kuwa, itafungua ubalozi wake katika mji wa Ramallah yalipo makao makuu ya Serikali ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina.
-
Majaji Wakuu wa Jumuiya ya Shanghai wamuenzi Shahidi Raisi
May 23, 2024 06:55Majaji Wakuu na Wenyeviti wa Mahakama za Juu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) wamenyamaza kimya kwa dakika moja kumuenzi Shahidi Ebrahim Raisi, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na maafisa wenzake walioaga dunia katika ajali ya helikopta iliyotokea Jumapili iliyopita katika mkoa wa Azarbaijan Mashariki, kaskazini magharibi mwa Iran.
-
Seneta wa Marekani aunga mkono ICC kutoa waranti wa kuwakamata viongozi wa Israel
May 23, 2024 04:14Seneta wa Marekani Bernie Sanders amesema anaunga mkono maombi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) Karim Khan ya kutaka viongozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wakamatwe na ameitaka Marekani iheshimu sheria za kimataifa.
-
Marekani kuipa Kenya hadhi ya mshirika wake mkuu asiye mwanachama wa NATO
May 23, 2024 03:50Rais Joe Biden wa Marekani anatarajiwa kuipa Kenya hadhi ya mshirika wake mkuu asiye mwanachama wa NATO wakati wa ziara ya kiserikali ya siku tatu ya Rais wa Kenya William Ruto nchini humo, ambaye amekaribishwa na Biden katika Ikulu ya White House mapema leo kabla ya mapokezi rasmi yatakayoanza kwa ukaguzi wa gwaride la heshima na kufikia kielele chake kwa dhifa ya kifahari ya chakula cha usiku.
-
Mwanasoka Muislamu atishiwa kuadhibiwa Ufaransa kwa kutoonyesha kwenye jezi yake beji ya kutetea LGBTQ
May 23, 2024 00:48Waziri wa michezo wa Ufaransa ametoa wito kwa klabu ya soka ya Monaco kupewa adhabu baada ya mchezaji wake kuficha kwenye jezi yake ujumbe wa kutetea 'ushoga' wakati wa mechi ya mwisho ya ligi ya nchi hiyo iliyofanyika siku ya Jumapili.