May 23, 2024 04:18 UTC
  • Mwanasoka Muislamu atishiwa kuadhibiwa Ufaransa kwa kutoonyesha kwenye jezi yake beji ya kutetea LGBTQ

Waziri wa michezo wa Ufaransa ametoa wito kwa klabu ya soka ya Monaco kupewa adhabu baada ya mchezaji wake kuficha kwenye jezi yake ujumbe wa kutetea 'ushoga' wakati wa mechi ya mwisho ya ligi ya nchi hiyo iliyofanyika siku ya Jumapili.

Michuano ya ubingwa wa soka wa Ufaransa iliandaa kampeni yake ya kila mwaka dhidi ya ubaguzi wakati wa mechi za mwisho mwishoni mwa juma, huku wachezaji kila timu wakiwa wamevalia beji inayoonyesha neno "homophobia" lenye maana ya uenezaji chuki dhidi ya ushoga.

Hata hivyo, kiungo wa timu ya Monaco, Mohamed Camara alifunika beji hiyo wakati timu yake iliposhinda mabao 4-0 dhidi ya Nantes, na pia aligomea picha ya pamoja ya kabla ya mechi ambapo wachezaji wote walisimama mbele ya beramu lililokuwa na ujumbe huohuo.

Waziri wa Michezo wa Ufaransa Amélie Oudéa-Castéra amedai kuwa hatua alizochukua Camara "hazikubaliki" na kutaka "adhabu kali" itolewe dhidi ya mchezaji huyo na klabu yake ya Monaco. Aurore Bergé, Waziri wa Fursa Sawa wa Ufaransa, naye pia amelaani Mohamed Camara kupitia mtandao wa kijamii wa X akiandika. “kuchukia wapenzi wa jinsia moja si maoni, ni uhalifu, na chuki dhidi ya wapenzi wa jinsia moja inaua. Mohamed Camara lazima aadhibiwe vikali. ”

Kocha wa Monaco Adi Hütter alisema baada ya mechi kuwa klabu hiyo inaunga mkono mpango wa ligi na kwamba hatua aliyochua Camara ni "chaguo la binafsi". Amesema, klabu hiyo itajadili suala hilo na Camara mwenyewe.

Huu ni msimu wa nne mfululizo ambapo vilabu vya soka vya Ufaransa vimetakiwa kutumia nambari za rangi ya upinde wa mvua, beji za mkononi au kwenye jezi zao kupitia upatu vitendo vichafu vya LGBTQ. Migogoro kama hiyo hutokea kila mwaka wakati wa ligi ya soka ya nchi hiyo.

Idrissa Gueye

Mnamo mwaka 2022, kiungo wa Everton mzaliwa wa Senegal, Idrissa Gueye, ambaye wakati huo alikuwa akiichezea PSG, alikataa kushiriki katika mechi ambayo wachezaji walitakiwa kuvaa jezi za rangi ya upinde wa mvua. Rais wa Senegal wakati huo Macky Sall alimuunga mkono Gueye, na kutangaza kwamba "imani yake ya kidini lazima iheshimiwe".

Mwaka jana pia, Nantes ilimpiga faini mshambuliaji wa Misri Mostafa Mohamed kwa sababu sawa na hizo. Wawili hao hawakushiriki katika mechi ya Jumapili. Mohamed Camara hakucheza katika mechi sawa na hiyo katika msimu uliopita.../

 

Tags