Jun 23, 2024 08:06 UTC
  • Radiamali ya Josep Borrell kwa shambulio la Wazayuni kwenye Ofisi ya Msalaba Mwekundu huko Gaza

Joseph Borrel Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya amelaani shambulio la utawala wa kigaidi wa Israel dhidi ya ofisi ya Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu katika huko Ukanda wa Gaza.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la ISNA Joseph Borrell amelaani mashambulizi ya utawala wa Kizayuni katika ofisi ya Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu katika Ukanda wa Gaza na kutaka uchunguzi huru ufanyike ili kuwawajibisha wahusika wa uhalifu huo.

Borrell amesisitiza kuwa Shirika la Msalaba Mwekundu lazima liwe na uwezo wa kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Mkataba Wa Geneva, ikiwa ni pamoja na kutoa misaada ya kibinadamu, kuwasaidia waathirika na kuweza kuwafikia wa wafungwa.

Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) ilitangaza siku ya Ijumaa katika taarifa kwenye akaunti yake ya mtandaoni kuwa ofisi ya shirika hili lisilo la kiserikali katika Ukanda wa Gaza na makazi ya wafanyakazi wake huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu yalishambuliwa na jeshi la Israel.

Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu  (ICRC)

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, jengo la ofisi ya Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu, ambako mamia ya raia waliokimbia makazi yao, wakiwemo wenzao wengi wa Kipalestina wa shirika hilo na familia zao wanaishi karibu na jengo hilo, limeharibiwa vibaya kutokana na shambulio hilo la Wazayuni, ambapo watu 22 wameuawa shahidi na wengine 45 wamejeruhiwa vibaya katika mashambulizi hayo yaliyofanywa na Israel huko Gaza.