May 24, 2024 02:36 UTC
  • Baada ya Colombia kuvunja uhusiano na Israel, sasa kufungua ubalozi wake Ramallah

Baada ya Colombia hivi karibuni kuvunja uhusiano wake na utawala haramu wa Israel, nchi hiyo sasa imetangaza kuwa, itafungua ubalozi wake katika mji wa Ramallah yalipo makao makuu ya Serikali ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina.

Luis Gilberto Murillo, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Colombia amesema kuwa, Rais Gustavo Petro Raus wan chi hiyo ametoa agizo la kufuunguliwa ubalozi wa nchini katika mji wa Ramallah ambao ndio mji mkuu wa Mamkala ya Ndani ya Palestina.

Mwanzoni mwa mwezi huu wa Mei, Colombia iliamua kuvunja uhusiano wake wa kidiplomasia na utawala wa Kizayuni wa Israel kutokana na vita vya kinyama na mauaji ya kimbari yanayoendelea kufanywa na utawala huo haramu dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.

Rais Gustavo Petro, ambaye ni mkosoaji mkubwa wa mashambulizi ya kikatili yanayofanywa na Israel huko Ghaza, alitangaza uamuzi huo alipohutubia maandamano ya maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi katika mji mkuu wa nchi hiyo Bogota.

 

Mnamo mwezi Oktoba 2023 pia, Rais wa Colombia alimshambulia vikali waziri wa vita wa utawala wa Kizayuni Yoav Gallant kwa kutumia lugha dhidi ya watu wa Gaza ambayo alisema ni sawa na waliyoitumia Wanazi kuhusu Wayahudi. Utawala wa Kizayuni uliamua "kusimamisha usafirishaji wa vifaa vya masuala ya usalama" kwa nchi hiyo ya Amerika ya Kusini.

Mwezi Februari mwaka huu, Rais Petro alisimamisha ununuzi wa silaha za Israel baada ya shambulio la kinyama la jeshi la utawala huo ghasibu dhidi ya Wapalestina wa Gaza, waliokuwa wamekusanyika kupokea msaada wa kibinadamu, akisema shambulio hilo "linaitwa mauaji ya kimbari.