May 25, 2024 02:04 UTC
  • Vikwazo vya China dhidi ya Marekani

ikiwa ni katika kukabiliana na mashinikizo ya vikwazo na pia uuzaji wa silaha za Marekani katika eneo la Taiwan, China imepitisha vikwazo dhidi ya makampuni 12 yanayuhusiana na viwanda vya kijeshi vya Marekani na wasimamizi wakuu wa mashirika hayo.

Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, makampuni hayo ya Marekani ni pamoja na Lockheed Martin, Raytheon na General Dynamicsna.

Kuchukuliwa vikwazo dhidi ya makampuni haya na serikali ya China kutajumuisha kuzuiliwa mali zao zilizoko nchini China na wakuregenzi wakuu wa makumpuni hayo kupigwa marufuku kuingia China.

Hatua ya China kuweka vikwazo hivyo dhidi ya makampuni muhimu zaidi ya viwanda vya Marekani ni muhimu kwa sababu kadhaa. Kwanza, inaonyesha kwamba China imefikia kiwango cha uhuru kamili na kujitegemea na wakati huo huo ina uwezo na inajiamini kiasi cha kuyawekea vikwazo makampuni ya Marekani na Magharibi na kwa msingi huo inatuma ujumbe wa wazi kuwa ina haki ya kutetea uhuru wake wa kitaifa. Pili, Marekani haiwezi tena kuilazimisha nchi kama China kufuata sera zake kwa kutumia silaha ya vikwazo. Nukta ya tatu ni kuwa, China imethibitisha kwa mara nyingine kivitendo kwamba Taiwan ni mstari wake mwekundu. Hakuna shaka kuwa China haitaruhusu Marekani kukisukuma kisiwa cha Taiwan kujitenga na China bara kwa kuimiminia misaada ya kijeshi serikali ya kisiwa hicho.

Zhu Hua, mtaalamu wa masuala ya kimataifa katika Kitivo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Chuo Kikuu cha Masuala ya Kigeni cha Beijing, anasema hivi kuhusiana na nukta hiyo: "Utekelezaji wa vikwazo vya China dhidi ya makampuni ya Marekani unaonyesha imani kubwa ya China kuhusu uwezo wake wa kukabibiliana na Marekani. Ni wazi kuwa China haiiogopi Maekani kuhusiana na suala hilo la vikwazo na iko tayari kukabiliana na hatua yoyote ile itakayochukuliwa na wakuu wa Washington.

Manowari ya Marekani karibu na kisiwa cha Taiwan

Sera yoyote ya vikwazo vya Marekani na uingiliaji wa nchi hii katika masuala ya ndani ya China ni ishara kwamba Marekani inatumia njia mbalimbali kuishinikiza China, ikiwa ni pamoja na masuala inayodai kuwa eti ni ya haki za binadamu, masuala ya biashara na kadhia ya Taiwan. Lakini hivi majuzi, kwa kuongeza misaada ya silaha kwa Taiwan na kushadidisha vikwazo dhidi ya makampuni ya Kichina, Marekani imeonyesha kuwa sio tu kwamba haizingatii sera ya China moja, bali pia inajaribu kuainisha mipaka ya China ili nchi hiyo kubwa isiwe kikwazo katika satwa ya kibeberu ya Marekani dunaini.

Kwa kuiuzia Taiwan silaha, Marekani imekiuka kikamilifu sera ya kimsingi ya ‘China Moja’ na hivyo kudhuru mamlaka ya kujitawala China. Kwa msingi huo, kupitia vikwazo ilivyoweka, China inajaribu kuishinikiza Marekani ibadilishe sera zake za uhasama dhidi ya nchi hiyo.

China imeonyesha mara kadhaa kuwa haina nia ya kuanzisha makabiliano ya kijeshi na Marekani na wala haiko tayari kuingia katika mtego wa mgogoro mkubwa na Marekani. Hii ni kwa sababu wakuu wa China wanafahamu vizuri kuwa lengo la Marekani ni kuihusisha China na migogoro au mivutano ya kijeshi ili kwa njia hiyo idhoofishe ustawi wake wa  kiuchumi. Kudidimia China kiuchumi bila shaka kutakuwa ni kwa maslahi ya Marekani.