-
Umaarufu wa Marekani barani Afrika waporomoka, China na Russia zavutia Waafrika wengi
Apr 24, 2024 23:13Utafiti wa hivi karibuni katika zaidi ya nchi 130 uliofanywa na shirika la uchunguzi wa maoni la Marekani la Gallup umebaini kuwa umashuhuri wa Marekani umeshuka katika nchi nyingi za bara Afrika.
-
Jamaica yatambua rasmi taifa la Palestina
Apr 24, 2024 23:02Jamaica inasema imeamua kuitambua rasmi Palestina kama taifa huku kukiwa na wasiwasi wa muda mrefu juu ya vita vya Israel vinavyoendelea katika Ukanda wa Gaza na mzozo mbaya wa binadamu katika eneo hilo lililozingirwa.
-
Borrell: Uharibifu wa Israel huko Gaza unazidi uliofanywa katika miji ya Ujerumani katika Vita vya Pili vya Dunia
Apr 24, 2024 08:54Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya amesema kuwa vita vya Israel dhidi ya Gaza vimesababisha uharibifu mkubwa kwenye miji ya eneo hilo kuliko ule uliosababishwa na Vita vya Pili vya Dunia kwenye miji ya Ujerumani.
-
Mwakilishi anayeiunga mkono Palestina ashinda katika mchujo wa wagombea viti vya Kongresi
Apr 24, 2024 08:32Summer Lee kutoka jimbo la Pennsylvania amefanikiwa kuibuka na ushindi katika uchaguzi wa wagombea wa Baraza la Wawakilishi la Marekani kwa kuungwa mkono kwa kura za wananchi wa Marekani wanaowatetea wananchi madhlumu wa Palestina licha ukwamishaji na vizuizi vya Lobi ya Kizayuni ya AIPAC.
-
Watu 5 wafariki dunia wakivuka English Channel, saa chache baada ya kuidhinishwa muswada wa Sunak
Apr 24, 2024 04:39Watu wasiopungua 5 wamekufa walipokuwa wakivuka njia ya majini ya English Channel, saa chache baada ya Uingereza kuidhinisha muswada wa kuwafukuza wahamiaji nchini humo na kuwapeleka Rwanda.
-
Ripoti: Nusu ya watu duniani wanazama katika madeni
Apr 24, 2024 03:19Ripoti mpya ya Shirika la Fedha la Maendeleo ya Kimataifa imefichua kuwa karibu nusu ya watu duniani wanaishi katika nchi ambako fedha zinazotolewa kulipa madeni zinazidi fedha za matumizi ya huduma za msingi za kijamii kkama elimu na afya.
-
Kamishna wa UN: Picha ya mtoto anayetolewa kwenye fuko la mama yake anayekata roho Ghaza ni zaidi ya tukio la vita
Apr 23, 2024 23:14Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa amekemea vikali mashambulio ya kinyama na ya mfululizo yaliyofanywa hivi karibuni na jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda Gaza na kuua zaidi wanawake na watoto.
-
Waziri wa Ulinzi wa Russia: Ukraine imeshapoteza karibu askari nusu milioni
Apr 23, 2024 23:13Waziri wa Ulinzi wa Russia Sergey Shoigu amesema, hasara za kijeshi ilizopata Ukraine za kuuawa askari wake tangu Februari 2022 hadi sasa zimefikia karibu wanajeshi 500,000.
-
Tume ya Haki za Binadamu ya Ulaya: Uingereza isitishe mpango wa kuwapeleka wahamiaji huko Rwanda
Apr 23, 2024 08:34Tume ya Kutetea Haki za Binadamu ya Ulaya, imetoa wito kwa Uingereza kutupilia mbali mpango wake wenye utata wa kuwatuma waomba hifadhi nchini Rwanda.
-
Chama cha Congress cha India chataka Modi achukuliwe hatua kwa matamshi yake ya dhidi ya Waislamu
Apr 23, 2024 08:02Chama cha Indian National Congress, ambacho ndicho kikubwa zaidi cha upinzani nchini India, kimewasilisha ombi kwa Tume ya Uchaguzi kikitaka kuchukuliwa hatua dhidi ya Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi, kwa kutoa matamshi ambayo Congress inasema "hayakubaliki kabisa" dhidi ya Waislamu nchini humo na yanakiuka sheria za uchaguzi.