Apr 24, 2024 12:02 UTC
  • Mwakilishi anayeiunga mkono Palestina ashinda katika mchujo wa wagombea viti vya Kongresi

Summer Lee kutoka jimbo la Pennsylvania amefanikiwa kuibuka na ushindi katika uchaguzi wa wagombea wa Baraza la Wawakilishi la Marekani kwa kuungwa mkono kwa kura za wananchi wa Marekani wanaowatetea wananchi madhlumu wa Palestina licha ukwamishaji na vizuizi vya Lobi ya Kizayuni ya AIPAC.

Kanali ya habari ya Sahab imearifu kuwa, Summer Lynn Lee mwakilishi wa Baraza la Wawakilishi la Marekani ameibuka na ushindi katika kinyang'anyiro cha mchujo kilichogharimu pakubwa cha wagombea wa chama cha Democrat katika wilaya ya 12 ya Pennsylvania katika uchaguzi wa Kongresi ya Marekani wa mwaka huu wa 2024.  

Baada ya Oktoba 7 mwaka jana, Lee alikuwa miongoni mwa sauti chache zilizojitokeza mapema zikitaka kusitishwa vita vya Israel dhidi ya Gaza; na kufuatia msimamo wake huo makundi yenye misimamo ya kuchupa mipaka yanayoihami Israel yalimtuhumu Bi Summer Lee kuwa amepuuza jamii ya Wayahudi na kudhoofisha sera za Rais Joe Biden katika eneo la Asia Magharibi.  

Vita vya Israel dhidi ya Gaza 

Msimamo huo wa Summer Lee wa kuwatetea wananchi wa Palestina na kupinga Uzayuni umemfanya aungwe mkono na wananchi katika kinyang'anyiro hicho cha uchaguzi. Summer Lee, mwakilishi wa chama cha Democrat katika Baraza la Wawakilishi la Marekani, katika moja ya jumbe zake katika mtandao wa X alisema: Kitendo cha kushambulia watu wa Gaza kwa mabomu kinapaswa kukosolewa na ni jinai ya kivita; na ndiyo maana sote tunapaswa kutoa wito wa kusitishwa kwa mapigano hivi sasa dhidi ya Gaza."

Tags