Oct 06, 2023 02:48 UTC
  • Wasiwasi wa Biden kuhusu kukatizwa misaada ya Ukraine

Mvutano wa ndani wa Warepublican umetatiza mazungumzo ya bajeti katika Baraza la Wawakilishi la Marekani umepelekea Ikulu ya White House kuwa na wasiwasi juu ya kuendelea kuunga mkono Kyiv kama kipaumbele kikuu cha siasa za kigeni za utawala wa Biden.

Kuhusiana na hilo, Rais Joe Biden wa Marekani siku ya Jumatano alibainisha wazi wasiwasi wake kwamba mvutano katika Bunge la Congress ya Marekani huenda ukavuruga upelekaji wa misaada ya nchi hiyo huko Ukraine.

Rais Joe Biden wa Marekani (kulia) akiwa na Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine

Katika kujibu swali kuhusu iwapo ana wasiwasi wa kutotimiza ahadi zake za kutuma msaada kwa Ukraine kutokana na  mivutano katika Bunge la Congress la Marekani, Biden amesema: Nina wasiwasi, lakini uungaji mkono wa wawakilishi wa pande zote mbili katika Baraza la Wawakilishi na Seneti unanipa uhakika wa kutatuliwa suala la kutolewa misaada kwa Ukraine.

Wasiwasi wa Biden kuhusu kuendelea misaada ya Washington kwa Kyiv kwa kuzingatia matukio ya hivi karibuni katika Baraza la Wawakilishi, na kuondolewa Kevin McCarthy, Spika wa Republican wa Baraza la Wawakilishi la Marekani katika nafasi hiyo, ulidhiri katika upigaji kura Jumanne, Oktoba 3 katika mivutano ya ndani kati ya Warepublican wenye msimamo mkali na wenye msimamo wa wastani. Wanachama wa Republican na wanaomunga mkono Trump hawakuridhika na utendaji wa McCarthy katika kushirikiana  na serkali ya Biden kwa ajili ya kuongeza deni na kupasisha bajeti ya muda mfupi. Kupasishwa mpango uliopendekezwa na McCarthy wa kusimamishwa kwa muda shughuli za serikali, bila shaka, kungeiletea matatizo serikali ya Biden ya kutotumwa misaada kwa Ukraine, ambalo lingelikuwa pigo kubwa kwa siasa za serikali ya Biden ya kuendelea kutoa misaada kwa Ukraine. Kwa hakika, Baraza la Wawakilishi, lilipasisha mswada wa muda, wa kuzuia kutofungwa shughuli za serikali ya shirikisho ya Marekani, ambayo ilitaka kuondolewa moja ya siasa muhimu za serikali ya Biden, ya kutoa msaada kwa Ukraine jambo ambalo lingekuwa pigo la wakati mmoja kwa rais wa Marekani na mwenzake wa Ukraine. Joe Biden hatimaye alitia saini muswada wa muda wa kuzuia kufungwa serikali kwa siku 45. Ingawa siasa hizo zilivutia wengi huko Washington lakini zilihatarisha moja ya siasa zake muhimu ambayo ni kuisaidia Ukraine.

Nukta muhimu ni kwamba Warepublican wenye itikadi kali katika Baraza la Wawakilishi la Marekani wanapinga vikali kuendelea kutolewa misaada ya Washington kwa Kyiv katika vita vyake na Russia na wanataka kusitishwa kwa misaada hjiyo na na fedha hizo zitumike katika masuala ya ndani, ikiwa ni pamoja na ufuatiliaji zaidi wa masuala ya mipaka.

Biden alikuwa ameomba Congress kuidhinisha dola bilioni 24 kama msaada wa ziada kwa Ukraine mnamo Julai 2023. Ikulu ya White House ilitangaza Jumanne kwamba kiwango cha sasa cha ufadhili wa muda kitaendelea kwa takriban miezi miwili zaidi, kumaanisha kuwa haitawezekana kuidhinisha msaada zaidi kwa Ukraine katika Bunge la Marekani katika kipindi cha miezi miwili ijayo.

Donald Trump

Suala muhimu ni kwamba, katika mazingira ya hivi sasa ya mvutano wa Warepublican wenye msimamo mkali na wenye msimamo wa wastani, uchaguzi wa spika ajaye wa Baraza la Wawakilishi uko katika hali isiyoeleweka vyema, na hata kama wawakilishi wa Republican watakubali na kumchagua spika mpya, takwa kuu la kuchaguliwa spika la kundi lenye itikadi kali ni kupunguza au kukata kabisa misaada kwa Ukrain. Wakati huo huo, msimamo wa hivi karibuni wa Donald Trump, rais wa zamani na mgombea mkuu wa chama cha Republican katika uchaguzi wa urais wa 2024, unasaidia kuimarisha nafasi ya mrengo wenye itikadi kali katika chama cha Republican. Trump amependekeza Washington isimamishe misaada yake kwa Ukraine, ambayo amesema ni dola bilioni 175, hadi Ulaya ilingane na Marekani katika kutuma misaada hiyo kwa nchi hiyo.

Tags