Jan 18, 2024 10:52 UTC
  • Ethiopia na Sudan zasusia mkutano wa Jumuiya ya IGAD

Ethiopia imesema mkutano wa Wakuu Jumuiya ya Maendeleo ya Kiserikali (IGAD) umefanyika leo Alhamisi huku ikiwa na mipango mengine. Wakati huo huo Sudan pia imedai kuwa haikushirikishwa katika ajenda ya mkutano huo.

Mivutano imeongezeka ndani ya jumuiya ya kikanda ya IGAD, kufuatia baadhi ya nchi wanachama wake kuonyesha waziwazi kutokua na imani na taasisi hiyo ya kikanda.

IGAD inazijumuisha  nchi za Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Somalia, Sudan Kusini, Sudan na Uganda.

Jumuiya ya kikanda ya IGAD 

Mapema wanachama wawili wa IGAD wameweka wazi kwamba hawatahudhuria Mkutano wa leo wa Wakuu wa nchi  wa jumuiya ya IGAD. Mkutano huo ulitazamia kuyapatia ufumbuzi masuala ya msingi yanayozikabili nchi  nchi wanachama.

Ethiopia kwa upande wake imesema  kuwa haitaweza kuhudhuria mkutano huo ikisema kuwa  yapo baadhi ya mambo yanayouingilia mkutano  huu tajwa.

Djibouti, ambayo ni Mwenyekiti wa jumuiya ya IGAD, tarehe 11 Januari 2024 ilitoa mualiko kwa nchi wanachama kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa leo wa Wakuu wa jumuiya hiyo ya kikanda. 

Mwaliko huo ulieleza kuwa mkutano wa Alhamisi ya leo utajikita katika  "masuala mawili makuu ambayo ni masuala yanayoendelea kati ya Jamhuri ya Shirikisho la Ethiopia na Jamhuri ya Shirikisho la Somalia na hali ya mambo huko Sudan."

Tags