Mar 13, 2024 07:45 UTC
  • Mahakama Uganda yapinga ombi la kusajiliwa kundi la LGBT

Mahakama moja nchini Uganda imetupilia mbali ombi la kundi moja la kutetea mahusiano ya kingono ya watu wa jinsia moja LGBT, lililotaka korti hiyo iilazimishe serikali ya Kampala itoe idhini ya kusajiliwa kwa kundi hilo.

Uamuzi huo wa jana Jumanne wa mahakama ya Uganda umetolewa kufuatia rufaa iliyowasilishwa na kundi hilo la Sexual Minorities Uganda (SMUG), baada ya korti nyingine ya chini ya nchi hiyo kupuuzilia mbali ombi hilo mwaka 2018.

Faili hilo liliwasilishwa na kundi hilo kwa mara kwanza katika Mahakama Kuu ya Uganda mwaka 2015, likitaka kuruhusiwa kuendesha shughuli zake eti kwa njia halali na kwa kufuata sheria.

Serikali ya Uganda mara kadhaa imelaani vikali hatua ya Magharibi ya kulazimisha ajenda ya mapenzi ya watu wa jinsia moja (LGBT) barani Afrika.

Nchi hiyo imekuwa ikivutana na nchi za Magharibi tangu ipasishe sheria hiyo kali ya kukabiliana na vitendo viovu vya maingiliano haramu ya watu wa jinsia moja.

Vita dhidi ya ushoga Uganda

Nchi za Magharibi pamoja na mashirika yake ya kifedha yameikatia Uganda misaada na kuinyima mikopo kutokana na nchi hiyo ya Afrika Mashariki kupasisha sheria ya kupinga vitendo vichafu vya ubaradhuli.

Miezi kadhaa iliyopita, Rais Yoweri Museveni wa Uganda alipasisha rasmi sheria ya kupiga marufuku nchini humo na kuwachukulia hatua kali wanaojihusisha na mahusiano ya kingono ya watu wa jinsia moja kwa mujibu wa Sura ya 91(3)(a) ya Katiba ya Uganda ya Mwaka 2015.

Tags