May 05, 2024 04:01 UTC
  • Watu wa Burkina Faso waandamamana kulaani Marekani kuingilia mambo yao

Idadi kubwa ya wananchi wa Burkina Faso wamekusanyika nje ya ubalozi wa Marekani katika mji mkuu wa nchi hiyo wakipinga tuhuma za maafisa wa Marekani dhidi ya jeshi la nchi hiyo.

Maandamano hayo yalikuja kufuatia ripoti ya Shirika la Haki za Binadamu (HRW) ambalo lilidai kuwa jeshi la nchi hiyo ya Kiafrika limewaua raia katika vijiji viwili mwezi Februari.

Siku ya Jumatatu, Marekani ilitoa taarifa ya pamoja na Uingereza, ikiitaka serikali ya Burkina Faso "kuchunguza kwa kina mauaji hayo na kuwawajibisha waliohusika".

Mamia ya waandamanaji walikusanyika siku ya Ijumaa nje ya ubalozi wa Marekani huko Ouagadougou, mji mkuu, ambapo waliilani Marekani kwa kwa kile walichokitaja kuwa ni tuhuma zisizo na msingi dhidi ya jeshi la nchi yao.

Wenye maduka na wafanyakazi wa sekta ya kibinafsi waliandamana kuelekea ubalozi wa Marekani wakiwa wanapeperusha bendera za Burkina Faso na Russia huku wakiimba nyimbo za kupinga ubeberu.

"Tumekuja kutoa ujumbe kwa Wamarekani ili kukomesha tuhuma zisizo na msingi dhidi ya majeshi yetu ambayo yanalinda nchi kwa gharama ya maisha yao," Mahamadou Ouedraogo, msemaji wa kundi lililoandaa maandamano hayo, alisema.

Serikali ya Burkina Faso hivi majuzi ilisitisha shughuli za mashirika kadhaa ya habari ya nchi za Magharibi, ikiwa ni pamoja na VOA na BBC kwa kurusha hewani tuhuma dhidi ya jeshiTaifa hilo la Afrika Magharibi ambalo halina bandari limekuwa lilikabiliana na magaidi wakufurishaji tangu mwaka 2015.