Vita vyaisababishia Sudan hasara ya zaidi ya dola bilioni 200 + Video
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i112714-vita_vyaisababishia_sudan_hasara_ya_zaidi_ya_dola_bilioni_200_video
Vita vya uchu wa madaraka baina ya majenerali wa kijeshi vinavyoendelea kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa, vimeusababishia uchumi wa Sudan, hasara ya zaidi ya dola bilioni 200.
(last modified 2025-12-07T11:27:20+00:00 )
Jun 09, 2024 03:18 UTC
  • Vita vyaisababishia Sudan hasara ya zaidi ya dola bilioni 200 + Video

Vita vya uchu wa madaraka baina ya majenerali wa kijeshi vinavyoendelea kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa, vimeusababishia uchumi wa Sudan, hasara ya zaidi ya dola bilioni 200.

Mwandishi wa televisheni ya al Alam nchini Sudan ameandaa ripoti maalumu kuhusu maafa yaliyosababishwa na vita baina ya majenerali wa kijeshi nchini humo pamoja na madhara ya ukame na kuripoti kuwa, uchumi wa Sudan umepata hasara ya zaidi ya dola bilioni 200 katika kipindi cha mwaka mmoja na kitu cha vita hivyo vya uchu wa madaraka.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, maeneo yaliyoangamizwa vibaya zaidi katika vita hivyo ni taasisi za umma, mabenki na masoko. 

 

Mwandishi wa televisheni ya al Alam amesema kwenye ripoti hiyo kwamba vita vya hivi sasa vya Sudan vimeathiri kila kitu na kuangamiza masoko makuu ya nchi hiyo kama Modurman ambayo sasa hivi yamebakia magovu matupu na hata kama kuna kitu kimebakia, basi wezi hawawezi kukibakisha salama.

Vita vya Sudan vimepoteza maisha ya maelfu ya wafanyabiashara. Mmoja wa wafanyabiashara hao ni Yusuf ambaye amekubali kufanyiwa mahojiano na mwandishi huyo wa televisheni ya al Alam na kusema kuwa, amekuwa akifanya biashara kwenye soko la Omdourman kwa zaidi ya miaka 30 lakini hivi sasa amefilisiwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe na dukani mwake hamjabakia chochote. 

Vilevile vita hivyo vya kugombania mbadaraka baina ya majenerali wa kijeshi vimezidisha mateso ya ukame na ukosefu wa mazao kiasi kwamba ripoti za kimataifa zinaonesha kuwa hivi sasa zaidi ya Wasudan milioni 18 wakiwemo watoto wadogo milioni 3.6 wanateseka kwa njaa.