Mawaziri wa Afya wa SADC kukutana kujadili Mpox
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i115418-mawaziri_wa_afya_wa_sadc_kukutana_kujadili_mpox
Mawaziri wa Afya wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) wanatarajiwa kukutana hivi karibuni kwa ajili ya kujadili virusi vya homa ya MPOX ambavyo vinaenea kwa kasi sasa katika maeneo tofauti ya dunia.
(last modified 2024-08-19T22:43:37+00:00 )
Aug 19, 2024 22:43 UTC
  • Mawaziri wa Afya wa SADC kukutana kujadili Mpox

Mawaziri wa Afya wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) wanatarajiwa kukutana hivi karibuni kwa ajili ya kujadili virusi vya homa ya MPOX ambavyo vinaenea kwa kasi sasa katika maeneo tofauti ya dunia.

Katibu Mtendaji wa SADC Elias Magosi amesema kuwa, mkutano wa mawaziri wa afya utaitishwa ili “kuwezesha utaratibu wa kukabiliana na ugonjwa huo, ambao umeenea katika zaidi ya nchi kumi za Afrika.

Wiki iliyopita, Shirika la Afya Duniani (WHO) liliitangaza Mpox kuwa "dharura ya afya ya umma" kwa mara ya pili sasa katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.

Kabla ya hapo pia, Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa barani Afrika CDC kilitangaza "dharura ya afya ya umma", kiwango chake cha juu zaidi cha tahadhari, juu ya mripuko wa Mpox unaoenea kwa kasi katika bara hilo, na kutoa wito wa kuchukuliwa hatua za kukomesha kusambaa kwake.

J

 

umla ya visa 38,465 vya ugonjwa huo, ambao zamani ulijulikana kama homa ya nyani, vimerekodiwa katika nchi 16 za Afrika tangu mwezi Januari 2022, pamoja na vifo 1,456, na ongezeko la 160% la kesi mwaka huu 2024 ikilinganishwa na mwaka uliopita, kulingana na data zilizochapishwa wiki iliyopita na Africa CDC.

Kesi za Mpox ziliripotiwa kwa mara ya kwanza wiki iliyopita katika nchi za Burundi na Rwanda baada ya kuripoti mripuko wa maradhi hayo DRC; huku kesi zaidi zikigunduliwa pia nchini Kenya na Jamhuri ya Afrika ya Kati.