Jul 25, 2016 11:18 UTC
  • Kuongezeka mgawanyiko wa kisiasa Sudan Kusini

Mgawanyiko wa kisaisa umeshadidi huko Sudan Kusini kufuatia Riek Machar kiongozi wa waasi wa nchi hiyo kumfukuza Taban Deng Gai kwa upande mmoja; na matamshi ya kiwanagenzi ya Deng Gai na sisitizo lake la kusalia katika nafasi yake kwa upande wa pili.

Gazeti la Sudan Tribune limeripoti kuwa mivutano ya kisiasa imeshtadi huko Sudan Kusini kiasi kwamba Riek Machar ametoa taarifa na kumtaarifu Rais Salva Kiir wa  nchi hiyo kuhusu kuachishwa kazi Deng Gai kama Waziri wa Madini katika serikali ya mpito ya nchi hiyo. 

Riek Machar Makamu wa Rais na ambaye pia ni kiongozi wa waasi wa zamani wa Sudan Kusini Jumatatu alitoa taarifa akimtaarifu Rais Kiir kuhusu kumuuzulu Deng Gai aliyekuwa Waziri wa Madini katika serikali ya mpito ya Sudan Kusini na akasema kuwa, atamteuwa shakhsia mwingine atakayechukua nafasi ya Deng akirejea Juba baada ya kudhaminiwa hali ya usalama na jeshi kutoka nje. Katika taarifa yake hiyo, Machar ameashiria juu ya kutumwa kikosi hicho cha jeshi cha nchi ya tatu kitakachowajumuisha  wanajeshi wa Kiafrika katika kalibu ya kikosi cha  askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa. 

 

Waziri wa Madini wa Sudan Kusini aliyefutwa kazi na Riek Machar 

Hata hivyo katika matamshi yake ya karibuni kabisa,Taban Deng Gai amesema hafahamu kuhusu agizo hilo la kuuzuliwa kwake na kusisitiza kuwa yeye akiwa kama mjumbe wa makundi ya upinzani anataka kuhitimishwa mapigano na kurejea amani na uthabiti huko Sudan Kusini. 

Wakati huo huo Nyarji Roman msemaji wa Riek Machar  ameitaja hatua hiyo ya Deng kuwa ni njama inayojiri huko Sudan Kusini dhidi ya Machar. Hii ni katika hali ambayo chama kinachoongozwa na Machar kimeituhumu serikali ya Juba kuwa inafanya juhudi za kumuainisha shakhsia atakayechukua nafasi ya Machar. Wanachama wa chama hicho wameeleza kuwa serikali ya Sudan Kusini inafanya jitihada za kuchochea hitilafu kati ya waasi wa zamani; huku wakisisitiza kuzidi kuwa na imani na kiongozi wao Riek Machar ambaye pia ni Makamu wa Rais wa nchi hiyo. 

 

Waasi wa zamani Sudan Kusini 

Waasi wa zamani walitangaza katika taarifa yao Ijumaa iliyopita kuwa Riek Machar Teny Dhurgon ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Sudan Kusini, angali ni Mkuu na Kamanda wa ngazi ya juu wa Harakati ya Ukombozi ya nchi hiyo. 

Taarifa ya waasi hao wa zamani imeongeza kuwa, kutekelezwa jitihada  au njama zozote ili kubadili fremu ya uongozi wa harakati hiyo ni jambo lisilokubalika kabisa; njama ambazo zinaweza kutoa pigo kubwa kwa makubaliano ya amani ya mwezi Agosti mwaka jana na kwa serikali ya umoja wa kitaifa ya Sudan Kusini.  Waasi hao wa zamani walisema kuwa jeshi la ukombozi wa Sudan Kusini linawaomba Salva Kiir na Jenerali Paul Malong Mkuu wa vikosi vya majeshi ya nchi hiyo wasititishe haraka iwezekanavyo  juhudi zao za kijeshi za kutaka kumfungulia mashtaka Riek Machar na matarajio hewa ya Taban Deng ya kutaka kuwa Makamu wa Rais. 

Itakumbukwa kuwa Makamu wa Rais wa Sudan Kusini Riek Machar aliondoka mji mkuu Juba baada ya kujiri mapigano yaliyotishia makubaliano ya kusaka amani waliyosaini mwaka jana kati ya serikali na upinzani ili kuhitimisha vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.  

 

 

 

 

Tags