Maelfu ya raia wamekuwa wakimbizi kaskazini mwa Kongo
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i12823-maelfu_ya_raia_wamekuwa_wakimbizi_kaskazini_mwa_kongo
Ofisi ya Uratibu wa Misaada ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa imetangaza kuwa, raia zaidi ya elfu 20 katika wilaya ya Tshopo katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kaskazini mwa nchi hiyo wamekuwa wakimbizi.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Aug 07, 2016 22:27 UTC
  • Maelfu ya raia wamekuwa wakimbizi kaskazini mwa Kongo

Ofisi ya Uratibu wa Misaada ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa imetangaza kuwa, raia zaidi ya elfu 20 katika wilaya ya Tshopo katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kaskazini mwa nchi hiyo wamekuwa wakimbizi.

Ofisi ya Uratibu wa Misaada ya Umoja wa Mataifa imeripoti kuwa raia elfu 23 katika kijiji cha Opienge katika eneo la Bafwasende katika wilaya ya Tshopo, kaskazini mwa Kongo wamekuwa wakimbizi kufuatia mapigano yaliyojiri kati ya makundi mawili ya waasi.  Ripoti ya Umoja wa Mataifa imeongeza kuwa wakimbizi hao wanaishi katika hali ngumu na wanakabiliwa na uhaba wa suhula muhimu kama chakula, dawa na na kadhalika.

Wakimbizi wa Kongo

Hii ni katika hali ambayo uwasilishaji wa huduma za kibinadamu kwa wakazi wa kijii cha Opienge unawezekana iwapo misaada ya kifedha itatolewa hususan misaada ya wafadhili kwa kuzingatia kuwepo upungufu wa wafanyakazi wa huduma za misaada ya kibinadamu katika mkoa huo ulioathiriwa na mapigano ya waasi.

Mapigano kati ya makundi mawili ya waasi yalianza tarehe 27 Juni hadi tarehe Pili Julai katika eneo la Bafaswende na yamewalazimisha maelfu ya watu kuyahama makazi yao.