UN: Makubaliano ya amani ya Kongo na Rwanda 'hayaheshimiwi'
Umoja wa Mataifa umesema kuwa makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Rwanda "hayaheshimiwi."
Huang Xi Mjumbe Maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya Eneo la Maziwa Makuu Barani Afrika amesema kuwa juhudi za amani za kimataifa zinapaswa kupongezwa na zinatia matumaini hata hivyo hadi sasa makubaliano ya kusimamisha vita yaliyofikiwa kati ya Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hayaheshimiwi.
Huang Xia amezitolea wito nchi za Eneo la Maziwa Makuu kuanza tena mazungumzo ya moja kwa moja na ya wazi, na kuchukuliwa hatua zote zinazohitajika kukomesha vita haraka iwezekanavyo.
Zenon Ngay Mukongo Mwakilishi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo katika Umoja wa Mataifa ameeleza kuwa kusitishwa uhasama, kuondoka wanajeshi wa Rwanda, wanajeshi hao kuacha kuwasaidia waachi wa M23 na kurejeshwa mamlaka ya serikali ya Kongo kwa maeneo yote yaliyovamiwa kutapelekea kufanyika mazungumzo ya kweli. ya amani.
Mzozo wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo umesababisha vifo vya maelfu ya watu na kupelekea mamilioni ya wengine kuhama makazi yao.
Mjumbe Maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya Eneo la Maziwa Makuu Barani Afrika amesisitiza kuwa amani ya kudumu inahitaji kushughulikiwa chimbuko na sababu za kimuundo za mgogoro wa mashariki mwa Kongo.