Bunge la Libya laakhirisha tena kikao cha kupasisha serikali mpya
Feb 17, 2016 00:05 UTC
Kikao cha kupiga kura ya kuwa na imani na serikali mpya ya umoja wa kitaifa ya Libya katika Bunge la Taifa la nchi hiyo linalotambuliwa rasmi na jamii ya kimataifa, kimeahirishwa tena.
Awali ilipangwa kuwa kikao hicho kingefanyika jana lakini kimeahirishwa. Mbunge Aisha al Aqouri wa Libya amesema kuwa wawakilishi wenzake 118 waliokuwepo bungeni hiyo jana walichukua uamuzi wa wa kumpa Waziri Mkuu wa Libya fursa ya hadi kufikia Jumanne ijayo kwa ajili ya kuarifisha mawaziri wa serikali yake.
Serikali mpya ya Libya ilitangazwa Jumapili iliyopita chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa. Serikali hiyo ina mawaziri 13 na mawaziri washauri 5.
Tags