Rais Mugabe atoa onyo kali kwa waandamanaji dhidi ya serikali yake
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i14042-rais_mugabe_atoa_onyo_kali_kwa_waandamanaji_dhidi_ya_serikali_yake
Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ametoa onyo kali kwa waandamanaji dhidi ya serikali yake nchi humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 27, 2016 02:52 UTC
  • Rais Mugabe atoa onyo kali kwa waandamanaji dhidi ya serikali yake

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ametoa onyo kali kwa waandamanaji dhidi ya serikali yake nchi humo.

Taarifa iliyotolewa na ikulu ya Rais Mugabe sanjari na kuwaonya waandamanaji imesema kuwa, maandamano hayo ya upinzani dhidi ya serikali hayatakuwa na faida yoyote. Katika taarifa hiyo Rais Mugabe amewatuhumu pia wapinzani kwa kusema kuwa, waandamanaji wanachoma matairi katika barabara kwa lengo la kutaka kutwaa uongozi nchini Zimbabwe na kuongeza kama ninavyonukuu: "Wanadhania kwamba kile kilichojiri miongoni mwa mapinduzi ya wananchi katika nchi za Kiarabu kitaweza tena kujiri nchini Zimbabwe." Mwisho wa kunukuu.

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe akihutubia taifa

Rais Mugabe ameyasema hayo katika hali ambayo Ijumaa ya jana polisi ya Zimbabwe ilitumia mabomu ya kutoa machozi katika kuwatawanya waandamanaji mjini Harare, mji mkuu wa nchi hiyo. Makumi ya polisi walivamia maandamano ya wananchi ambao walikuwa wakipiga nara za kutaka kufanyiwa marekebisho mfumo wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2018.

Polisi wa Zimbabwe wakikabiliana na waandamanaji 

Uchaguzi wa rais nchini Zimbabwe umepangwa kufanyika mwishoni mwa mwaka 2018 na kuna uwezekano rais huyo mkongwe akagombea tena.