Makumi ya Wamalawi watiwa mbaroni nchini Msumbiji
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i15121-makumi_ya_wamalawi_watiwa_mbaroni_nchini_msumbiji
Raia zaidi ya 60 wa Malawi wametiwa mbaroni nchini Msumbiji na kutupwa jela wakihusishwa na vitendo vya kuvuruga usalama wa nchi hiyo.
(last modified 2026-02-05T09:20:29+00:00 )
Sep 11, 2016 09:40 UTC
  • Makumi ya Wamalawi watiwa mbaroni nchini Msumbiji

Raia zaidi ya 60 wa Malawi wametiwa mbaroni nchini Msumbiji na kutupwa jela wakihusishwa na vitendo vya kuvuruga usalama wa nchi hiyo.

Raia hao wa Malawi wametiwa mbaroni baada ya kushadidi mapigano baina ya waasi wa Renamo na vikosi vya serikali vya chama tawala cha Frelimo. Raia hao wametiwa mbaroni na vikosi vya usalama vya Msumbiji katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo wakiwa katika shughuli zao za kawaida.

Wizara ya Mashauri ya Kigeni na Ushirikiano wa Kimataifa ya Malawi imetangaza kuwa, inafuatilia kadhia hiyo ili kujua hatima ya raia wake hao.

Baadhi ya waliotiwa mbaroni wameziambia duru za habari kwamba, wameendelea kuzuiliwa na vikosi vya usalama vya Msumbiji bila ya kuelezwa makosa yao huku wakiteswa na kupigwa.

Vikosi vya usalama vimeimarisha ulinzi nchuini Msumbuji

Wakati huo huo, watu wasiopingua wanane wamefariki dunia kusini mashariki mwa Msumbuji na makumi ya wengine kujeruhiwa kufuatia mapigano kati ya vikosi vya usalama na wanamgambo wanaofungamana na chama cha upinzani cha Renamo.

Msumbiji imeendelea kushuhudia hali ya kulegalega kisiasa, kijamii na kiuchumi licha ya kupita miongo minne tangu ijipatie uhuru, huku juhudi za kuleta mwafaka baina ya chama tawala cha Frelimo na wapinzani wa chama cha Renamo zikiambulia matupu.