Wakimbizi wa Sudan Kusini zaidi ya 600 wafukuzwa Kongo
Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kimearifu kuhusu kufukuzwa wakimbizi wa Sudan Kusini zaidi ya 600 huko mashariki kaskazini mwa Kongo.
Kikosi hicho kimeeleza kuwa askari jeshi wa kikosi hicho kimewafukuza wakimbizi wa Sudan Kusini 634 katika eneo la mbuga ya Garamba katika mkoa wa Haut-Uele kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kufuatia oparesheni iliyofanywa na kikosi hicho cha kulinda amani nchini Kongo kuanzia tarehe 17 mwezi uliopita wa Agosti hadi sasa. Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa kilichoppo Kongo kimeongeza kuwa wakimbizi wengine wa Sudan Kusini karibu 134 bado wamesalia katika eneo la mbuga ya Garamba na kwamba wanapaswa kuondoka katika eneo hilo. Kikosi hicho kimesisitiza katika taarifa yake kuwa oparesheni hiyo imetekelezwa kwa lengo la kuwasaidia watu walioko katika hali ngumu na vile vile kuwasaidia raia ambao kuna uwezekano wakawa wahanga wa kuwepo wakimbizi wa Sudan huko Kongo. Maelfu ya wakimbizi wa Sudan Kusini wamekimbilia nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakiepa mapigano yanayojiri nchini kwao.