Sep 15, 2016 15:57 UTC
  • Waislamu Nigeria waandamana wakitaka Sheikh Zakzaky aachiwe huru

Waislamu nchini Nigeria kwa mara nyingine tena wameandamana wakitaka kuachiwa huru haraka iwezekanavyo Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya nchi hiyo Sheikh Ibrahim Zakzaky.

Mamia ya Waislamu wa Nigeria waliendeleza maandamano yao dhidi ya jeshi na askari usalama wa nchi hiyo wakitaka kuachiwa huru Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya nchi hiyo ambaye hali yake ya kiafya inazidi kuwa mbaya.

Ripoti zinasema kuwa, watu wa karibu na ndugu wa Sheikh Zakzaky wameeleza wasiwasi wao kuhusu hali mbaya ya kiafya ya kiongozi huyo wa Kiislamu na kuzitolea mwito taasisi husika kufuatia haraka suala hilo.

Sheikh Ibrahim Zakzaky baada ya kujeruhiwa na jeshi la Nigeria 

Jumuiya za Kutetea Haki za Binadamu zimekuwa zikikosoa na kulalamikia miamala iliyo dhidi ya binadamu ya jeshi na askari usalama wa Nigeria dhidi ya Waislamu wa Kishia katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.

Weledi wa mambo wanaamini kuwa upuuzaji wa serikali ya Nigeria na jeshi la nchi kwa matakwa ya kisheria ya Waislamu wa Kishia hauwezi kuhalalishwa kivyovyote na kwamba Sheikh Ibrahim Zakzaky anapaswa kuachiwa huru haraka iwezekanavyo.

Tags