Al Sisi: Jeshi la Misri lina nguvu
Rais wa Misri ameashiria kuwa tayari vikosi vya jeshi la nchi hiyo na kudai kuwa iwapo italazimu vikosi hivyo vya Misri vitasambazwa katika maeneo yote ya nchi hiyo katika muda wa masaa sita tu.
Rais Abdel Fattah al Sisi ameongeza kuwa, serikali ya Misri ina mpango wa kuliweka jeshi lake katika hali ya utayarifu ili iwapo kutakuwa na ulazima vikosi vya jeshi hilo visambazwe katika maeneo yote ya nchi hiyo katika muda wa masaa sita. Rais wa Misri amebainisha kuwa, serikali ya nchi hiyo ina vikosi vya ulinzi na Wizara ya Mambo ya Ndani yenye nguvu na kwamba hakuna yoyote anayeweza kuidhuru nchi hiyo. Rais al Sisi ameeleza kuwa, Misri imefanikiwa pakubwa katika mapambano dhidi ya ugaidi.
Rais wa Misri siku kadhaa zilizopita pia alidai akiwa ziarani mjini New York Marekani kuwa nchi yake ina uhusiano mzuri na utawala wa Kizayuni. Hii ni katika hali ambayo fikra za waliowengi huko Misri zinamtambua Rais Abdel Fattah al Sisi kuwa ni kiongozi aliyeingia madarakani kwa njia ya mapinduzi ambaye alipuuza matokeo ya uchaguzi wa Rais wa nchi hiyo mwaka 2012 na kumuondoa kijeshi madarakani Muhammad Morsi Rais wa kwanza wa Misri aliyechaguliwa kwa njia ya demokrasia.