Russia yatoa pendekezo la kusuluhisha mgogoro wa Libya
Russia yapendekeza kuwa msuluhishi katika mgogoro wa Libya
Abdulrahman al Swehili mmoja wa viongozi wa kisiasa wa Libya hivi karibuni alifanya mazungumzo na Mjumbe Maalumu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia huko Tripoli ambapo katika mazunguzo hayo, mjumbe huyo alieleza kuwa, nchi yake inamtaka kiongozi huyo wa kisiasa wa Libya ashiriki katika mazungumzo na vikao vya mapendekezo vinavyosimamiwa na Rais Vladimir Putin wa Russia, na Mawaziri wa Ulinzi na wa Nje wa nchi hiyo ili kupanua wigo wa makubaliano ya kisiasa huko Libya.
Wakati huo huo, Mjumbe Maalumu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia amesema kuwa nchi hiyo inajizuia kuzipatia silaha pande zinazozozana Libya kwa sababu hatua hiyo ni marufuku kwa mujibu wa sheria za kimataifa.
Al Swehili pia amekaribisha pendekezo hilo la Russia na kuwataka viongozi wa nchi hiyo kutekeleza majukumu yao na kuzidisha jitihada ili kupatikane amani na uthabiti huko Libya. Katika upande mwingine, vikosi vya Libya vimewazingira magaidi wa kundi la Daesh ndani ya eneo moja katika mji wa Sirte katika harakati za kuyakomboa maeneo yote ya mji huo.