Ujerumani yazidi kujikita kijeshi nchini Niger
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i16954-ujerumani_yazidi_kujikita_kijeshi_nchini_niger
Ujerumani imeimarisha kuwepo kwake kijeshi nchini Niger kwa kuanzisha kituo cha jeshi la anga katika mji mkuu wa nchi hiyo Niamey.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 08, 2016 00:34 UTC
  • Ujerumani yazidi kujikita kijeshi nchini Niger

Ujerumani imeimarisha kuwepo kwake kijeshi nchini Niger kwa kuanzisha kituo cha jeshi la anga katika mji mkuu wa nchi hiyo Niamey.

Balozi wa Ujerumani nchini Niger Bernd von Münchow-Pohl, amesema kituo hicho cha kwanza jeshi la anga la Ujerumani kimeanzishwa nchini Niger kwa madhumuni ya kutoa msaada na uungaji mkono kwa vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa vilivyotumwa nchini humo MINUSMA.

Kwa mujibu wa balozi huyo wa Ujerumani, Niger ni mshirika  muhimu kwa Berlin katika mapambano dhidi ya ugaidi na  katika kukabiliana na wimbi la wahajiri haramu na kwamba hivi sasa ukurasa mpya wa ushirikiano wa pande mbili umefunguliwa baina ya nchi hizo.

Münchow-Pohl ameashiria umuhimu wa eneo la kistratijia la Sahel barani Afrika na kusisitiza juu ya utayari wa kijeshi wa Ujerumani wa kutekeleza hatua zaidi nchini Niger.

Balozi wa Ujerumani nchini Niger, Bernd von Münchow-Pohl

Uamuzi wa kuanzishwa kituo cha kwanza cha kijeshi cha Ujerumani nchini Niger umechukuliwa katika hali ambayo mnamo mwezi Mei mwaka huu serikali ya Berlin ilitangaza kuwa imekubali kupanua iwgo wa kuwepo kwake kijeshi katika nchi hiyo ya Kiafrika.

Balozi wa Ujerumani nchini Niger aidha ametangaza kuwa mnamo siku zijazo Kansela Angela Merkel wa Ujerumani atafanya safari ya kuitembelea Niger.../