Iran yauenzi mchango wa Waafrika katika harakati ya Ashura
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i17188-iran_yauenzi_mchango_wa_waafrika_katika_harakati_ya_ashura
Mkuu wa Kitengo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Tanzania amesema John bin Huwai ni jani la dhahabu la Waafrika katika mapambano ya Ashura.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 11, 2016 04:39 UTC
  • Iran yauenzi mchango wa Waafrika katika harakati ya Ashura

Mkuu wa Kitengo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Tanzania amesema John bin Huwai ni jani la dhahabu la Waafrika katika mapambano ya Ashura.

Ali Baqeri, ameyasema hayo katika maombolezo ya Muharram yaliyofanyika katika msikiti wa Imam Ali (AS) uliopo eneo la Kigamboni mjini Dar es Salaam na kubainisha kuwa kwa kujitoa mhanga na kuuawa shahidi katika kukabiliana na maadui wa Uislamu, John bin Huwai, mmoja wafuasi watiifu wa Imam Hussein (AS) katika hamasa ya Karbala ni jani la dhahabu na la kujivunia kwa Waafrika katika mapambano ya Ashura.

Huku akibainisha kuwa Imam Hussein (AS) alipambana  ili kuwaokoa wanadamu na dhulma na ujinga, Mkuu wa Kitengo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Tanzania ameongeza kuwa Chuo na Madrasa ya Ashura ni chuo cha uokovu kwa ajili ya mataifa yote na zama zote na kimekuwa kipenzi cha wapigania uhuru na watu walionyongeshwa katika zama zote za historia.

Ashura, mapambano ya ukombozi wa mwanadamu

Baqeri aidha amebainisha kuwa mafundisho ya Ashura yanawiyana na fitra na maumbile safi ya mwanadamu na kwamba mataifa yanayodhulumiwa kama ya watu wa Afrika yana ukuruba na mfungamano maalumu na Ashura.

Msikiti wa Imam Ali (AS) uliopo katika eneo la Kigamboni mjini Dar es Salaam umejengwa na Waislamu wa madhehebu ya Shia, ukiwa pia na madrasa ya Qur'ani ya Bibi Fatimatu-Zahra pamoja na nyumba ya mwalimu wa madrasa hiyo.

Maombolezo ya Imam Hussein (AS) na tukio adhimu la Ashura yamefanyika pia katika madrasa ya al-Batul iliyoko eneo la Mbagala mjini Dar es Salaam.

Madrasa hiyo iliyoko chini ya taasisi ya Az-Zahra ya nchini Tanzania imejengwa na wanachuo wanawake waliohitimu masomo yao ya juu hapa nchini Iran.../