Boko Haram yasababisha maelfu ya watoto wa Nigeria kuwa wakimbizi
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i1777-boko_haram_yasababisha_maelfu_ya_watoto_wa_nigeria_kuwa_wakimbizi
Zaidi ya watoto 6,500 wako katika hatari ya kupoteza maisha yao kutokana na baa la njaa linalowakabili, katika kambi za wakimbizi wa ndani nchini Nigeria.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 23, 2016 04:51 UTC
  • Boko Haram yasababisha maelfu ya watoto wa Nigeria kuwa wakimbizi

Zaidi ya watoto 6,500 wako katika hatari ya kupoteza maisha yao kutokana na baa la njaa linalowakabili, katika kambi za wakimbizi wa ndani nchini Nigeria.

Sule Mele, Mkuu wa Bodi ya Huduma za Afya Jimbo la Borno amesema kesi zaidi ya 6,444 za watoto kukabiliwa na utapiamlo ziliripotiwa katika kambi hizo mwaka jana 2015, huku kesi zingine 25,500 za magonjwa yanayotokana na athari za kutopata lishe bora zikiripotiwa. Mele amesema watoto 459 walio na umri wa kati ya mwaka 1-5 walipoteza maisha yao wakiwa katika kambi hizo mwaka jana kutokana na magonjwa ya kuambukiza kama vile kutapika, kuendesha na ukambi.

Takwimu zinaonyesha kuwa, watu zaidi ya 20,000 wameuawa na wengine zaidi ya milioni 2.5 wamelazimika kuwa wakimbizi katika nchi yao, tangu kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram lianzishe hujuma zake nchini Nigeria mwaka 2009.