Seneta wa Marekani afichua uhusiano wa Washington na Daesh
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i18199-seneta_wa_marekani_afichua_uhusiano_wa_washington_na_daesh
Seneta mmoja wa chama cha Republican nchini Marekani amesema uhusiano kati ya Washington na kundi la kigaidi la Daesh umechangia kusambaratisha usalama na utulivu katika eneo la Mashariki ya Kati.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 26, 2016 11:30 UTC
  • Seneta wa Marekani afichua uhusiano wa Washington na Daesh

Seneta mmoja wa chama cha Republican nchini Marekani amesema uhusiano kati ya Washington na kundi la kigaidi la Daesh umechangia kusambaratisha usalama na utulivu katika eneo la Mashariki ya Kati.

Katika mahojiano na kanali ya televisheni ya Press TV, Richard Hayden Black, Seneta wa jimbo la Virginia amesema vita vinavyoendelea nchini Syria vingekuwa vimemalizika iwapo Marekani ingejiweka kando baada ya Russia kuingia katika nchi hiyo ya Mashariki ya Kati kwa lengo la kuyatokomeza magenge ya kigaidi.

Seneta Richard Black wa Marekani

Seneta huyo amesema vita vya Syria vilipamba moto baada ya shirika la ujasusi la Marekani CIA kusafirisha silaha zake kutoka Libya hadi Uturuki na kisha hadi Syria, silaha ambazo hatimaye zilifika mikononi mwa makundi ya kigaidi likiwemo kundi la matakfiri wa Daesh.

Wakati huo huo, Seneta wa Jimbo la Virginia amewapongeza wananchi wa Yemen kwa kusimama kidete dhidi ya Saudi Arabia licha ya kuwa ni nchi ndogo na masikini. Amesema binafsi anasikitishwa na namna Washington inavyouunga mkono utawala wa kifalme wa Riyadh katika hujuma zake za kinyama nchini Yemen na kuongeza kuwa, ulimwengu sasa umetambua wazi uovu na jinai za kivita za Saudia dhidi ya watu masikini wa Yemen.

Magaidi wa Daesh wanaaminika kupata misaada ya kifedha na silaha kutoka Marekani na Saudia

Richard Hayden Black, Seneta wa jimbo la Virginia kadhalika ameeleza kughadhibishwa kwake na namna vyombo vya habari vya Magharibi vinavyofanya juu chini kuonyesha kuwa eti Iran ni muungaji mkono wa ugaidi na kusisitiza kuwa, falsafa ya Uwahabi ambayo chimbuko lake ni Saudia ndiyo imechangia kuenea kwa kasi ugaidi kote duniani.