Niger: Makundi yenye misimamo mikali yapigwe vita
(last modified Fri, 04 Nov 2016 07:41:27 GMT )
Nov 04, 2016 07:41 UTC
  • Niger: Makundi yenye misimamo mikali yapigwe vita

Serikali ya Niger imesema kuwa, makundi yenye silaha na yenye misimamo mikali huko kaskazini mwa Mali yanahusika na machafuko na mashambulizi ya hivi karibuni nchini humo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Niger, Ibrahim Yacouba amesema kuwa mashambulizi matatu yaliyotokea huko  Mali katika kipindi cha siku kumi ni jambo linalotia wasiwasi. Ibrahim Yacouba amesema kuwa makundi yenye silaha huko kaskazini mwa Mali ndiyo yanayosababisha hali ya mchafukoge nchini Niger sababu hakuna kundi lolote lenye misimamo ya kuchupa mipaka katika ardhi ya Niger.

Ibrahim Yacouba, Waziri wa Mambo ya Nje wa Niger

Ibrahim Yacouba ametaka kuchukuliwa hatua kali ili kuyaangamiza makundi hayo huko Mali na kuongeza kuwa, bila ya kuchukuliwa hatua kali na kufanyika mashambulizi dhidi ya makundi hayo nchi nyingine za Kiafrika za eneo la Sahel pia zitakumbwa na janga la ugaidi.

Niger imekuwa ikikabiliwa na mashambulizi ya wanamgambo wa kundi la Boko Haram wa Nigeria na makundi mengine yenye silaha ya Mali.

Magaidi wa kundi la kitakfiri la Boko Haram

 

Tags