Baraza la Usalama kushirikiana na serikali ya Somalia dhidi ya uharamia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i19213-baraza_la_usalama_kushirikiana_na_serikali_ya_somalia_dhidi_ya_uharamia
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limesisitiza kuendeleza ushirikiano na serikali ya Somalia katika kupambana na uharamia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 10, 2016 10:16 UTC
  • Baraza la Usalama kushirikiana na serikali ya Somalia dhidi ya uharamia

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limesisitiza kuendeleza ushirikiano na serikali ya Somalia katika kupambana na uharamia.

Kupitia azimio lililopigiwa kura na wajumbe wote, Baraza la Usalama la UN kwa mara nyingine limezitaka nchi wanachama, mataifa na kadhalika asasi za kieneo kuendeleza ushirikiano na serikali ya Mogadishu katika kupambana na uharamia. Aidha azimio hilo sanjari na kuonyesha masikitiko kufuatia kuendelea harakati za uharamia wa baharini katika pwani ya Somalia, limesema kuwa uharamia, machafuko na ukosefu wa amani nchini humo vimeshadidi na hivyo kuongezeka kiwango cha jinai na ufisadi.

Maharamia wanaohatarisha usalama wa bahari ya Somalia

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limezitaka nchi zote kupitia sheria na mikataba ya kitaifa, kuchukua hatua zenye taathira kwa ajili ya kudhamini usalama wa taifa, uharamia na pia utakatishaji fedha. Hii ni katika hali ambayo mwezi Julai mwaka huu Umoja wa Mataifa ulitoa ripoti rasmi ambayo ilionyesha kwamba, wimbi la uharamia na wizi wa kutumia silaha katika maji ya Somalia vimepungua na kufikia kiwango cha chini zaidi kuanzia mwaka 1995 hadi sasa.

Maharamia wanaohatarisha usalama wa bahari 

Katika upande mwingine tarehe 15 Oktoba, viongozi wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika walikutana mjini Lome, mji mkuu wa Togo kwa ajili ya kujadili njia za kupambana na ugaidi, uharamia, magendo ya binaadamu na madawa ya kulevya sanjari na kuinua kiwango cha usalama wa bahari na ustawi wa nchi za bara hilo. 

Jeshi la Somalia likipiga doria dhidi ya maharamia