Misri yaunga mkono mapambano ya serikali za Syria, Iraq dhidi ya magaidi
Rais wa Misri ametangaza kuwa, nchi yake inaunga mkono majeshi ya nchi za Iraq na Syria katika mapambano yao dhidi ya ugaidi.
Abdul Fattah al Sisi ametilia mkazo suala la kuunga mkono mapambano ya majeshi ya Iraq na Syria dhidi ya makundi ya kigaidi na kusema kuwa, kuna udharura wa kukabiliana ipasavyo na magaidi na kukata vyanzo vinavyoyawezesha kupata silaha na zana za kivita.
Al Sisi amesema kuwa msimamo wa Cairo kuhusu mgogoro wa Syria ni kuunga mkono matakwa ya wananchi, kulinda ardhi yote ya nchi hiyo na vilevile jitihada za kupatikana mwakafa wa kisiasa wa kukomesha mapigano nchini humo.
isil
Msimamo huo wa serkali ya Misri wa kuliunga mkono jeshi la Syria unapingana na ule wa nchi kadhaa za Kiarabu kama Saudi Arabia na Qatar ambazo kwa miaka kadhaa sasa zimekuwa zikiyasaidia kwa hali na mali makundi ya kigaidi yanayopigana na jeshi na wananchi wa Syria.