Wanachama 100 wa Boko Haram waangamizwa Nigeria
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i2092-wanachama_100_wa_boko_haram_waangamizwa_nigeria
Operesheni ya pamoja ya majeshi ya Nigeria na Cameroon imefanikiwa kuangamiza wanachama 100 wa kundi la kigaidi na kitafkiri la Boko Haram , kaskazini mashariki wa Nigeria.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 28, 2016 04:30 UTC
  • Wanachama 100 wa Boko Haram waangamizwa Nigeria

Operesheni ya pamoja ya majeshi ya Nigeria na Cameroon imefanikiwa kuangamiza wanachama 100 wa kundi la kigaidi na kitafkiri la Boko Haram , kaskazini mashariki wa Nigeria.

Jenerali Jacob Kodji, Kamanda mwandamizi wa jeshi la Cameroon amenunukuliwa na shirika la habari la Associated Press akisema kuwa wanachama hao wa Boko Haram wameuawa katika operesheni ya pamoja ya kulikomboa eneo la Kumshe, yapata kilomita 15 kutoka mpakani mwa Nigeria na Cameroon. Kamanda huyo ameongeza kuwa, mamia ya mateka wameokolewa katika operesheni hiyo wakiwemo wasichana wadogo ambao walikuwa wanapokea mafunzo ya kuwa walipuaji mabomu wa kujitolewa muhanga. Kundi la Boko Haram limepanua mashambulizi yake kutoka Nigeria hadi katika nchi jirani za Chad, Cameroon na Niger. Inadaiwa kuwa kuna wanamgambo 8700 wa Boko Haram kwenye eneo hilo. Watu zaidi ya 20,000 wameuawa na wengine zaidi ya milioni 2.5 wakilazimika kuwa wakimbizi ndani na nje ya nchi tangu kundi la Boko Haram lianzishe hujuma zake nchini Nigeria mwaka 2009.