Dec 20, 2016 14:37 UTC
  • Nigeria yatilia mkazo ustawi na maendeleo ya kiuchumi magharibi mwa Afrika

Rais wa Nigeria ametilia mkazo ustawi na maendeleo ya kiuchumi kwa maslahi ya nchi za eneo la Magharibi mwa Afrika.

Rais Muhamadu Buhari wa Nigeria amesema, kuna udharura wa kutekelezwa mipango mbalimbali ya kiuchumi katika eneo la magharibi mwa Afrika ili kuondokana na mporomoko wa uchumi hadi kufikia mwishoni mwa mwaka ujao.  

Rais wa Ngeria amebainisha kuwa, kuimarisha uhusiano wa kiuchumi  kunaweza kuwa sababu ya kunawiri uchumi wa nchi za Kiafrika na ametilia mkazo suala la kupanuliwa nyanja za uchumi barani Afika hususan katika nchi ambazo zimeathirika vibaya na uchumi unaotegemea pato la mafuta ya petroli. 

Rais Buhari na wakuu wa Ecowas 

Nigeria ambayo imekuwa ikizingatiwa kama nchi muhimu na yenye pato kubwa zaidi barani Afrika, katika miaka ya hivi karibuni imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali za kiusalama, kisiasa na kiuchumi ambazo zimewaathiri pakubwa wananchi na serikali ya nchi hiyo. 

Tags