Magaidi wasafishwa kikamilifu katika mji wa Halab Syria, wananchi washerehekea + Video
Mji wa Halab yaani Aleppo huko kaskazini mwa Syria hivi sasa umesafishwa kikamilifu baada ya magaidi kufurushwa katika mji huo baada ya kuteka baadhi ya maeneo yake na kufanya jinai kwa muda wa zaidi ya miaka minne.
Komandi Kuu ya jeshi la Syria jana usiku ilitangaza kuwa, kufurushwa kikamilifu magaidi katika mji wa Halab na kurejeshwa amani katika mji huo ni mafanikio makubwa na ni hatua ya kistratejia. Kama lilivyosema jeshi la Syria, ushindi huo ni nukta adhimu katika mapambano dhidi ya ugaidi na ni pigo kubwa kwa njama za magaidi na waungaji wao mkono.
Komandi Kuu ya jeshi la Syria imesisitiza kuwa, mafanikio hayo makubwa ni motisha yenye nguvu kwa ajili ya kuendelezwa majukumu ya jeshi la taifa katika vita dhidi ya ugaidi na kurejesha amani na utulivu huko Syria.
Taarifa ya jeshi la Syria imeongeza kuwa, ushindi lilioupata jeshi hilo huko Aleppo ni sisitizo kuhusu nguvu lilizonazo jeshi la Syria na vikosi waitifaki wake katika mapambano dhidi ya makundi ya kigaidi; na vile vile ni ishara ya kuanza ukurasa mpya wa kumalizwa kikamilifu ugaidi katika ardhi yote ya Syria.
Komandi kuu ya jeshi la Syria kwa mara nyingine tena imeyataka makundi yote yenye silaha kuweka chini zao, kwa sababu jeshi hilo litaendeleza mapambano yake hadi kukombolewa sehemu ya mwisho ya ardhi ya Syria.
Mara baada ya kutangazwa kukombolewa kikamilifu mji wa Halab, wananchi wa nchi hiyo wamemiminika barabarani na kufanya sherehe usiku kucha.