Waislamu wa Nigeria waendelea kupigania Sheikh Zakzaky aachiwe huru
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i22318-waislamu_wa_nigeria_waendelea_kupigania_sheikh_zakzaky_aachiwe_huru
Waislamu wa Nigeria wamezidisha jitihada zao za kutaka kuachiwa huru haraka iwezekanavyo Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya nchi hiyo pamoja na mke wake.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 28, 2016 23:10 UTC
  • Waislamu wa Nigeria waendelea kupigania Sheikh Zakzaky aachiwe huru

Waislamu wa Nigeria wamezidisha jitihada zao za kutaka kuachiwa huru haraka iwezekanavyo Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya nchi hiyo pamoja na mke wake.

Waislamu wa Nigeria na viongozi wa Harakati ya Kiislamu ya nchi hiyo wanafanya juhudi za kufanya mashauriano ya kisiasa na viongozi wa serikali ili kutekelezwa haraka hukumu ya mahakama ya kumuachia huru Sheikh Ibrahim Zakzaky Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria na mke wake. Mahakama moja ya Nigeria imetangaza rasmi kuwa Sheikh Zakzaky na familia yake siku 20 zijazo watakabidhiwa kwa maafisa wa polisi. Hii ni katika hali ambayo kuachiwa huru Sheikh Zakzaky na familia yake ni hukumu ya kisheria ambayo hata hivyo faili lake limefika hadi katika vyombo vya sheria vya Nigeria kwa mujibu wa tuhuma ziziso sahihi na zilizo kinyume na uhakika wa mambo.

Sheikh Ibrahim Zakzaky mara baada ya kujeruhiwa na wanajeshi wa Nigeria mwaka uliopita 

Idara za usalama za Nigeria hivi karibuni zilipuuza hukumu ya mahakama ya nchi hiyo iliyotaka kuachiwa huru haraka kiongozi huyo wa Harakati ya Kiislamu ya nchi hiyo na mke wake na kuzuia pia kiongozi huyo kupewa huduma za matibabu. Itakumbukwa kuwa mwaka jana wanajeshi wa Nigeria waliivamia Husseiniya ya Harakati ya Kiislamu ya nchi hiyo na kuwauwa mamia ya Waislamu waliokuwepo mahala hapo. Aidha wanajeshi hao walimjeruhi vikali Sheikh Zakzaky na kumpeleka kusikojulikana.