Jamii ya Nigeria yapindukia watu milioni 190
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i22459-jamii_ya_nigeria_yapindukia_watu_milioni_190
Wakala wa Taifa wa Takwimu nchini Nigeria umetangaza kuwa jamii ya watu wa nchi hiyo imepindukia watu milioni 190.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 31, 2016 00:18 UTC
  • Jamii ya Nigeria yapindukia watu milioni 190

Wakala wa Taifa wa Takwimu nchini Nigeria umetangaza kuwa jamii ya watu wa nchi hiyo imepindukia watu milioni 190.

Taarifa iliyotolewa na wakala huo imesema kuwa, jamii ya watu wa Nigeria imefikia watu milioni 190 na laki tatu na kwamba jimbo la Kano lililoko kaskazini mwa nchi hiyo ndilo lenye jamii kubwa zaidi ya watu. Vilevile imesema mji wa Lagos ambao ndio mkubwa zaidi nchini Nigeria una wakazi milioni 12.

Hata hivyo viongozi wa jiji hilo kubwa zaidi la Nigeria wanasisitiza kuwa tangu miaka 10 iliyopita hakujafanyika sensa makini nchini humo na kwamba wakazi wa mji huo mkuu wa kibiashara na kiuchumi ni milioni 22. 

Lagos, Nigeria

Umoja wa Mataifa unasema mji wa Lagos ambao katika muongo wa 1970 ulikuwa na jamii ya watu mioni moja na laki nne ndio mji mkubwa zaidi wa Nigeria. Mwaka 2012 jamii ya wakazi wa Lagos ilizidi ile ya wakazi wa mji wa Cairo nchini Misri ambao wakati huo walikadiriwa kuwa watu milioni 11. 

Sensa ya mwisho ilifanyika nchini Nigeria mwaka 2006 ambapo nchi hiyo ilikuwa na jamii ya watu milioni 140 na laki nne.