Kudhoofika nguvu ya magaidi nchini Nigeria
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i25486-kudhoofika_nguvu_ya_magaidi_nchini_nigeria
Waziri wa Ulinzi wa Nigeria amesema kuwa kundi la Boko Haram limedhoofika baada ya kuundwa kikosi cha kijeshi cha pamoja cha mataifa kadhaa cha kupambana na hujuma za kundi hilo.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Feb 22, 2017 08:11 UTC
  • Kudhoofika nguvu ya magaidi nchini Nigeria

Waziri wa Ulinzi wa Nigeria amesema kuwa kundi la Boko Haram limedhoofika baada ya kuundwa kikosi cha kijeshi cha pamoja cha mataifa kadhaa cha kupambana na hujuma za kundi hilo.

Meja Jenerali Abayomi Olonisakin amesema kuwa mashambulizi na uwezo wa kundi la wanamgambo wa Boko Haram umepungua sana tangu kuundwa kikosi cha kijeshi cha pamoja cha kieneo cha mataifa kadhaa kwa kifupi MNJTF. Meja Jenerali Abayomi Olonisakin Waziri wa Ulinzi wa Nigeria ameongeza kuwa, kunapaswa kuzidishwa ushirikiano na mawasiliano kati ya kikosi hicho katika kutekeleza oparesheni dhidi ya kundi la Boko Haram. Waziri wa Ulinzi wa Nigeria ameyasema hayo katika ufunguzi wa mkutano wa nchi wanachama wa kamisheni ya kieneo ya Eneo la Maziwa Makuu (LCBC) huko Abuja mji mkuu wa nchi hiyo. 

Nchi zilizoathiriwa na mashambulizi ya kundi la kigaidi la Boko Haram 

Naye Lamidi Adeosun Kamanda wa kikosi hicho cha pamoja cha kieneo cha kukabiliana na Boko Haram amesema kuwa pamoja na kuwa Boko Haram imepoteza udhibiti wake katika baadhi ya maeneo, lakini kundi hilo bado halijaangamizwa kikamilifu na kwamba kikosi hicho cha kieneo kina muda wa kuweza kurejesha amani ya kudumu katika eneo la Ziwa Chad.