Askari wa kimataifa watuhumiwa kufanya uhalifu DRC
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i25600-askari_wa_kimataifa_watuhumiwa_kufanya_uhalifu_drc
Kamati ya nidhamu ya askari wa Umoja wa Mataifa wanaolinda amani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imesema kuwa, askari wa umoja huo wanatumuhimiwa kufanya vitendo visivyo vya kimaadili mwaka 2016 nchini Kongo.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Feb 25, 2017 00:45 UTC
  • Askari wa kimataifa watuhumiwa kufanya uhalifu DRC

Kamati ya nidhamu ya askari wa Umoja wa Mataifa wanaolinda amani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imesema kuwa, askari wa umoja huo wanatumuhimiwa kufanya vitendo visivyo vya kimaadili mwaka 2016 nchini Kongo.

Adama Ndao, mratibu wa kamati hiyo amesema, mwaka 2016 kuliripotiwa kesi 15 za vitendo vya uvunjifu wa maadili vinavyodaiwa kufanywa na askari wa kimataifa wa kulinda amani huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Aidha mratibu huyo wa kamati ya nidhamu ya askari wa Umoja wa Mataifa wanaolinda amani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ametaka wahojiwe raia, wanajeshi, serikali na askari wa kulindi amani wa Umoja wa Mataifa kuhusu suala hilo.

Wanawake na watoto wadogo, wahanga wakuu wa unyanyasaji wa kijinsia mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

 

Mwezi Machi 2016, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilitoa azimio la kuwabana zaidi askari wa kulinda amani ambao wanafanya uhalifu na vitendo visivyo vya kimaadili katika nchi yoyote ile ulimwenguni. 

Katika ripoti yake ya hivi karibuni Umoja wa Mataifa ulisema kuwa, mwaka uliopita wa 2016, vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu viliongezeka kwa asilimia 30 ikilinganishwa na mwaka wa kabla yake yaaani wa 2015 huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.