Kongo yaiomba Guinea Conakry iisaidie kutatua mgogoro wa kisiasa
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i26334-kongo_yaiomba_guinea_conakry_iisaidie_kutatua_mgogoro_wa_kisiasa
Ujumbe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo umeelekea Guinea Conakry ukitaka kushiriki Rais wa nchi hiyo katika kuupatia ufumbuzi mgogoro wa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 13, 2017 10:51 UTC
  • Kongo yaiomba Guinea Conakry iisaidie kutatua mgogoro wa kisiasa

Ujumbe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo umeelekea Guinea Conakry ukitaka kushiriki Rais wa nchi hiyo katika kuupatia ufumbuzi mgogoro wa nchi hiyo.

Felix Tshisekedi, Katibu Mkuu wa muda wa chama cha Umoja kwa Ajili ya Demokrasia na Maendeleo ya Jamii (UDPS) cha Kongo ambaye ndiye mwenyekiti wa ujumbe wa nchi hiyo ulioelekea Guinea Conakry amesema baada ya kufanya mazungumzo na Rais Alpha Conde wa nchi hiyo kuwa, safari ya ujumbe huo inafanyika kwa lengo la kupata njia za utatuzi wa mgogoro wa kisiasa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo baada ya kuakhirishwa uchaguzi wa Rais wa nchi hiyo. 

Felix Tshisekedi, Mwenyekiti wa ujumbe wa Kongo ulioelekea Guinea Conakry 

Felix Tshisekedi amesema kuwa uchaguzi wa rais wa nchi hiyo ulipasa kufanyika mwaka jana na kuhitimisha kipindi cha urais wa Rais Joseph Kabila.

Kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa Disemba 31 mwaka jana, Rais Joseph Kabila atabakia madarakani hadi utakapofanyika uchaguzi wa Rais na Bunge mwezi Disemba mwaka huu licha ya kumalizika muhula wake wa uongozi.

Wakati huo huo kutaundwa serikali ya mwaka mmoja ya kipindi cha mpito na shakhsia kutoka mrengo wa upinzani ndiye atakayekuwa waziri mkuu wa serikali hiyo.