48 wapoteza maisha katika maporomoko ya udongo jalalani Ethiopia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i26338-48_wapoteza_maisha_katika_maporomoko_ya_udongo_jalalani_ethiopia
Watu wasiopungua 48 wakiwemo watoto 15 wamefariki dunia katika maporomoko ya udongo yaliyotokea kwenye dampo kubwa la takataka nje kidogo ya mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa. Hayo yameelezwa na msemaji wa Halmashauri ya mji wa Addis Ababa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 13, 2017 11:00 UTC
  •  48 wapoteza maisha katika maporomoko ya udongo jalalani Ethiopia

Watu wasiopungua 48 wakiwemo watoto 15 wamefariki dunia katika maporomoko ya udongo yaliyotokea kwenye dampo kubwa la takataka nje kidogo ya mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa. Hayo yameelezwa na msemaji wa Halmashauri ya mji wa Addis Ababa.

Itafahamika kuwa mamia ya watu wamekuwa wakiishi katika eneo hilo la jalala la Reppi lenye umri wa miaka 50 wakisaka chakula na vitu vingine wanavyoweza kuviuza kama vile mabaki ya vyuma n.k.

Amare Mekonen msemaji wa Halmashauri ya mji mkuu, Addis Ababa amesema juhudi za uokoaji zinaendelea ili kuwasaka watu ambao bado hawajulikani walipo tangu kutokea maporomoko hayo ya udongo hapo juzi.

Juhudi za uokoaji zikiendelea katika dampo hilo la taka lililoporomoka Addis Ababa 

Watu wengine 20 wamapatiwa matibabu hospitali. Mekonen amesema kuwa, watu ambao walikuwa wakiishi katika eneo hilo la dampo la taka hivi sasa wamehamishiwa katika vituo vya vijana katika maeneo mengine ya Addis Ababa.